HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, November 2, 2012

mjini shule na mjini chuo kikuu: cheki changa la macho hili alilopigwa huyu mtu

 Katika pita pita zangu za kila siku mitaani nikakutana na mwanadada mmoja (hakutaka sura yake ionekane hadharani) akiwa analia na kusaga meno kwa machungu ya kutapeliwa hela zake kiasi cha shilingi laki nne (fedha za kimatumbi) na majamaa waliojitambulisha kuwa ni wafanya biashara ya madini kutoka kwenye hiyo kampuni ionekanayo hapo kwenye kikaratasi kilichokuwa kimebandikwa kwenye bahasha.Dada huyo aliingia mkenge na kutoa hela haraka haraka kwa kuamini kuwa kaula mchana mchana tena kweupeeee,baada ya kuonyeshwa kifuko kilichokuwa ndani ya bahasha chenye madini ya dhahabu daraja la kwanza.sasa kasheshe iliibuka pale jamaa walipotoweka machoni mwake na ndipo akaona huo ndio mwanya wa yeye kuchunguza kwa makini kilichopo ndani ya bahasha aliyopewa ili ajihakikishie ule ulaji wa fasta fasta aliopewa na jamaa.lakini alichokiona kwa umakini ndani ya bahasha hiyo,ilikuwa ni lazima alie na kusaga meno.hebu cheki picha za chini na utabaini.
 alipofungua ndani,mzigo ulikuwa hivi na hapa ndipo aliposhtuka na nusura presha impande.
 kuendelea kufungua zaidi akuna na madini haya ya dhahabu ya mchanga na mkaa.
na mwisho wa mchezo ndio ilikuwa hivi.yaani kwa chezo hili,kweli mjini ni zaidi ya uijuavyo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad