HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, November 9, 2012

Bendi ya Msondo Ngoma yakabidhiwa Vifaa Vipya vya Muziki kutoka Konyagi

 Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Tanzania Distilleries Ltd ambao ni watengenezaji wa kinyaji cha Konyagi,David Mgwasa (wa tatu kulia) akikabidhi sehemu ya vifaa vya Muziki kwa viongozi wa Bendi ya Muziki wa Dansi nchini ya Msondo Ngoma (Baba ya Muziki) vilivyotolewa na Kampuni yake kwa ajili ya kuuendeleza muziki wa Dansi hapa nchini.Makabidhiano haya yamefanyika jioni ya leo katika Viwanja vya Leaders,Kinondoni jijini Dar es salaam.Wengine Pichani toka kulia ni Meneja Mauzo TDL,Joseph Chibehe,Meneja wa Konyagi, Martha Bangu,Maalim Muhidin Gurumo,Said Mabela a.k.a Daktari,Roman Mng'ande na Shaaban Dede ambao ni wanamuziki wa Msondo Ngoma Band.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Tanzania Distilleries Ltd ambao ni watengenezaji wa kinyaji cha Konyagi,David Mgwasa (kulia) akikabidhi gitaa kwa Mwanamuziki Mkongwe wa Bendi ya Msondo Ngoma,Mzee Said Mabela (kushoto) ikiwa ni sehemu ya vifaa vya muziki vilivyotolewa na Konyagi kwa bendi hiyo,jijini Dar es Salaam jioni ya leo.Katikati ni Kiongozi wa Bendi hiyo,Maalim Muhidin Gurumo.
Wanamuziki wa Bendi ya Msondo Ngoma wakiwa kwenye picha ya Pamoja na viongozi wakuu wa Kampuni ya Tanzania Distilleries Ltd ambao ni watengenezaji wa kinyaji cha Konyagi mara baada ya kukabidhiwa vifaa vipya vya Muziki.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Tanzania Distilleries Ltd ambao ni watengenezaji wa kinyaji cha Konyagi,David Mgwasa (kulia) akizungumza machache mara baada ya kumalizika kwa zoezi la Makabidhiano ya Vifaa vya Muziki na Bendi ya Msondo Ngoma katika hafla iliyofanyika jioni ya leo kwenye viwanja vya Leaders,Kinondoni Jijini Dar es Salaam.Katikati ni Kiongozi wa Bendi hiyo,Maalim Muhidin Gurumo na kushoto ni Kiongozi Msaidizi wa Bendi hiyo,Mzee Said Mabela.
Kiongozi Msaidizi wa Bendi ya Msondo Ngoma,Mzee Said Mabela akitoa shukrani zake za dhati kwa Uongozi wa Konyagi ikiwa ni kwa niaba ya Bendi yake mada baada ya kukabidhiwa vifaa vipya vya Muziki kutoka Konyagi.
Bendi ya Muziki wa Dansi ya Msondo Ngoma chini ya Uongozi wake Maalim Muhidin Gurumo ikifanya vitu vyake jioni ya leo mara baada ya kukabidhiwa zana mpya za kazi kutoka Konyagi.
Ni furaha tupu kwa wanamuziki wa Msondo Ngoma.
Wanamuziki kazini.
sehemu ya Vifaa hivyo.

1 comment:

Post Bottom Ad