Waziri
wa Uchukuzi,Dkt. Harrison Mwakyembe akifungua mkutano wa pili wa
Lojistiki Afrika,katika Hotel ya Serena.Mkutano huo wa siku mbili
umewakutanisha wataalamu mbalimbali kujadili namna bora ya kuboresha
Lojistiki katika sekta ya Usafiri.
Mkuu
wa chuo Cha Taifa cha usafirishaji(NIT), Mhandisi. Dkt. Zacharia
Mganilwa,akitoa salamu zake wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa wa pili wa
Logistiki Afrika,Mkutano huo unafanyika katika hotel ya Serena,na
utafayika kwa siku Mbili huku ukijikita zaidi katika kuboresha Lojistiki
katika usafiri wa Reli.
Waziri
wa Uchukuzi,Dkt Harrison Mwakyembe akisikiliza kwa makini mada
Iliyoeleza umuhimu wa kutumia usafiri wa Reli na namna ambavyo ukitumiwa
vizuri unaweza kuongeza pato la Taifa, katika Mkutano wa Pili wa
Lojistiki Afrika, mkutano huo wa Siku mbili umewakutanisha wataalamu
mbalimbali kutoka Afrika na Nje ya Afrika.Kulia kwake ni Naibu Katibu
Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi,Bw. John Mndogo(aliyevaa miwani),Na kulia kwa
Naibu Katibu Mkuu ni Mkuu wa Chuo Cha Taifa Cha
Usafirishaji,Mhandisi,Dk. Zacharia Mganilwa.
Baadhi
ya wajumbe walioshiriki kwenye mkutano wa Pili wa Lojistiki Afrika
unaofanyika kwenye hotel ya Serena jijini Dar es Salaam.Mkutano huo
ulioanza leo unawakutanisha wataalamu mbalimbali wa sekta ya
usafirishaji kutoka ndani na nje ya Nchi,wataalamu hao watajadili Mada
mbali mbali za kuboressa lojistiki katika Usafirishaji kwa muda wa siku
mbili.
Waziri
wa Uchukuzi,Dkt Harrison Mwakyembe(wa tano kutoka kushoto),akiwa katika
picha ya Pamoja na wataalamu mbalimbali walioshiriki katika Mkutano wa
Pili wa Lojistiki Afrika.Mkutano huo wa siku mbili unafanyika katika
hotel ya Serena jijini Dar es Salaam na umewakutanisha wataalam
mbalimbali wa sekta ya Usafiri kutoka ndani na nje ya nchi.
No comments:
Post a Comment