Warembo wa Redd's Miss Tanzania 2012,wakiwa kwenye picha ya pamoja mchana huu katika kambi yao iliopo kwenye hoteli ya Geraffe,Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.Jumla ya Warembo 30 wameingia kwenye kambi hiyo kujiandaa ya kinyang'anyiro
cha kumsaka Mrembo atakaemlithi,Salha Israel ambaye anashikilia Taji
hilo hivi Sasa,ambapo fainali za mwaka huu zitafanyika Novemba 3,katika
hoteli ya Blue Peal,Ubungo Plaza jijini Dar.
Baadhi ya Warembo wa Redd's Miss Tanzania wakibadirisha mawazo wakati wakielekea kwenye chakula cha Mchana wa leo kwenye hoteli ya Geraffe,Mbezi Beach jijini Dar.
Warembo
wa Redd's Miss Tanzania wakionyesha umahiri wao wa kutembea (catwork)
mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) walioitembelea kambi hiyo
leo kwenye hoteli ya Geraffe,Mbezi Beach jijini Dar.
Warembo wakiwa kwenye kambi yao.
Baadhi ya Warembo wa Redd's Miss Tanzania wakiwa katika pozz tofauti tofauti ya picha.
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakiwa katika mazungumzo na Warembo wa Redd's Miss Tanzania,waliopo
kwenye kambi yao iliyopo kwenye hoteli ya Geraffe,Mbezi Beach jijini
Dar es salaam leo waliopowatembelea na kuzungumza nao maswala mbali mbali juu ya mashindano hayo.
Assallaam Aleykhum Ankal!
ReplyDeleteNadhani hili shindano la Redds Miss Tanzania limepoteza maana! Ukiangalia kwa makini utagundua kuwa washiriki wake wengi kuanzia katika vitongoji hadi katika ngazi ya finali ni wale ambao ama wameshindwa kutoka katika tasnia nyinginezo kama vile elimu, usanii nk sasa imekuwa kama vile ngoja tujaribu na huku! tofauti na miaka ya nyuma ambapo ushindani ulikuwa kwa kiwango kikubwa!! i.e. uzao wa kina Aina Maeda, Mariam Ikowa, Shose Sinare, Jokate Mwegelo, Wema Sepetu, Irene Kiwia,Saida Kessy, Happiness Magese, Nargis Mohamed, Faraja Kotta na wengineo! Leo hii unakwenda kuangalia Redds Miss Tanzania unakutana na wasichana ambao pia utawakuta wako katika biashara ya kuuza miili yao Seacliff Hotel, Kempiski, Jolly Club, J. B. Belmont, Maisha and Billicanas club! Hivi kwa utaratibu huu Uncle Hashim, Bosco, Makoye na Ramesh mnadhani ni nani atakubali kumruhusu binti yake aje kushiriki mashindano yenu? Tafakarini na mje na Plan mpya! nadhani Plan A imeshafeli mje na mtazamo mpya kwenye Jamii!! Ni wazo tu la kuboresha tasnia ya urembo Tanzania angalau tuweze kupata mwakilishi bora katika mashindano ya Miss World na pia kioo bora cha jamii nyumbani na africa mashariki na africa kwa ujumla!! Wasalaam!
shark_ham@yahoo.co.uk
nashauri muwaulize maswali muhimu yenye kuonyesha uelewa wa ma-miss, ili tupate miss kichwa atakaye re-present nchi vizuri, siyo miss mrembo wa muonekano lakini kichwani zero.
ReplyDeleteHakuna kitu hapo...Toka na Nancy Sumary hadi leo naona wanacheza tu
ReplyDeletewarembo wamependeza ila tatizo nguo zao. naomba kujua kwa wadau hivi kuwa miss lazima uwe na mavazi yanayo acha baadhi ya sehemu za mwili wazi?
ReplyDeleteHao wanatafuta vyeti vya kuchakachuliwa tu. wakishamaliza mashindano kila mmoja kashapata mabwana kama 20.
ReplyDeletena mimi nakuunga mkono, inakuwaje warembo kumi na sita wote wanaonyesha maoungo yao? huu umiss ni lazima wakae uchi? ukiangalia maandalizi mengine kutoka nchi mbalimbali utaona maadili ya jamii yanazingatiwa sana. Jaribuni kuwalea mabinti zetu katika maadili mazuri ili wawe mama wazuri wa kesho, tupate kizazi chenye hekima kwa maisha yajayo. Mama akivaa kaptula fupi kiasi hicho, mtoto wake si atavaa chupi kabisa. Na wala mama huyu hatauliza.
ReplyDelete