Mkuu
wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bandera , Oktoba mosi mwaka huu alifanya
ziara ya kikazi ya siku mbili katika Wilaya mpya ya Gairo.
Katika
ziara hiyo, iliyomchukua kufika hadi Kata ya Chanjale, ambapo moja ya
mambo ambayo aliyashuhudia ni suala la uharibifu mkubwa wa maliasili ya
misitu kunakofanywa na baadhi ya watanzania wenye tamaa ya kuhitaji
fedha za haraka.
Hata
hivyo Msitu wa hifadhi ya asili wa Kumbulu ,umeharibiwa vibaya kutokana
na ukataji wa miti ovyo , uchomaji wa mkaa na upasuaji wa mbao ,
vitendo hivyo vikomeshwe mara m oja.
Mkuu
wa Mkoa wa Morogoro,Joel Bendera pamoja na ujumbe wake wakiangalia
lundo la Magogo yaliyokuwa yamekusanywa sehemu moja kwa ajili ya
kuchomwa moto.
Askari Polisi wa Wilaya ya Gairo akifanya kazi ya kuharibu tanuli lililokuwa likichoma mkaa.
Msitu wa Hifadhi ya Asili wa Kumbulu ukiwa katika hatari ya kutokomezwa.
Wananchi
wa kijiji cha Namba 30,kijiji cha Kumbulu wakimsikiliza kwa makini Mkuu
wa Mkoa wa Morogoro,Joel Bendera (hayupo pichani) juu ya hali ya
uharibufu wa Mazingira.
No comments:
Post a Comment