Meneja
wa Kinywaji cha Redds Original,Victoria Kimaro akizungumza na Waandishi
wa Habari (hawapo pichani) katika Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo
jijini Dar es Salaam leo wakati wa kutangaza zawadi ya Mshindi wa Taji
la Reddd's Miss Tanzania 2012. Katikati ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino
International Agency ambao ni waandaaji wa Miss Tanzania, Hashim
Lundenga na Kushoto ni Katibu Mkuu wa Kamati ya Miss Tanzania,Bosco
Majaliwa.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Lino International Agency ambao ni waandaaji wa Miss
Tanzania, Hashim Lundenga akizungumza na waandishi wa habari (hawapo
pichani) katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es Salaam
leo wakati wa kutangaza zawadi za Mshindi wa Shindano la Redd's Miss
Tanzania 2012. Kulia ni Meneja wa Kinywaji cha Redd's Original, Victoria
Kimaro.
Meneja wa Kinywaji cha Redds Original,Victoria Kimaro akizungumza na
Waandishi wa Habari (hawapo pichani) katika Ukumbi wa Idara ya Habari
Maelezo jijini Dar es Salaam leo wakati wa kutangaza zawadi ya Mshindi
wa Taji la Reddd's Miss Tanzania 2012. Katikati ni Mkurugenzi wa Kampuni
ya Lino International Agency ambao ni waandaaji wa Miss Tanzania,
Hashim Lundenga na Kushoto ni Katibu Mkuu wa Kamati ya Miss
Tanzania,Bosco Majaliwa.waliosimama nyuma ni baadhi ya washiriki wa Redd's Miss Tanzania 2012.
Kampuni
ya TBL kupitia kinywaji chake cha Redds Original ambao ndio Mdhamini
mkuu wa shindano la Redds Miss Tanzania 2012, leo tunatangaza zawadi kwa
washiriki wote wanaowania taji la Redds Miss Tanzania 2012.
Akizungumza
na waandishi wa Habari Jijini Dar Es Salaam Mkurugenzi wa kampuni ya
LINO AGENCY Hashim Lundenga alisema katika fainali za shindano la Redds
Miss Tanzania 2012 zitafanyika tarehe 3 Novemba 2012 katika ukumbi wa
Blue Pearl Hotel, (Ubungo Plaza) jijini Dar es salaam ambapo ni
shindano linaloshirikisha washiriki 30 kutoka mikoa mbalimbali ya
Tanzania.
Leo
hii tunapenda kuchukua nafasi hii kuwatangazia rasmi kuwa katika
fainali ya Redds Miss Tanzania mwaka zawadi zitakuwa kama ifuatavyo
1) Mshindi wa Kwanza atapata zawadi ya pesa taslimu shs: 8,000,000/- pamoja na gari
2) Mshindi wa pili atapata zawadi ya pesa taslimu shs: 6,200,000/-
3) Mshindi wa tatu atapata zawadi ya pesa taslmu shs: 4,000,000/-
4) Mshindi wa nne atapata zawadi ya pesa taslimu shs; 3,000,000/-
5) Mshindi wa tano atapata zawadi ya pesa taslimu shs: 2,400,000/-
6) Mshindi wa sita hadi wa 15 kila mmoja atapata shs: 1,200,000/-
7) Washiriki wengine wote waliobaki kila mmoja atalipwa shs: 700,000/-
Katika
shindano hilo ambalo ndani yake kuna mashindano mengine madogo [Fast
Tract] tayari washiriki 3 wameshajipatia tiketi ya kuingia katika [Top
15 Finalist]
Washiriki hao ni Lucy Stephano – Miss Photogenic
Magdalena Roy – Top Model
Mary Chizi – Top Sport Woman
Shindano dogo lingine limepangwa kufanyika siku ya Ijumaa tarehe 26
Oktoba 2012 la kumtafuta mrembo wenye Kipaji. Miss Talent.
Na tarehe 28 Oktoba 2012 atapatikana Miss Personality.
Nae
Meneja wa kinywaji cha Redds Original Bi Victoria Kimaro amesema huu ni
wakati sahihi wa kumpata mshindi biomba mwenye vigezo sahihi hivyo
kuwataka wapenzi wote wa tasnia ya urembo na wapenda maendeleo kote
nchini kujianda kupata tiketi za kushudia fainali hiyo mapema ili kuweza
kupata fursa ya kupata burudani mbalimbali.
Kwa
kweli shindano la mwaka huu tunatarajia kuwa litafana sana hasa kwa
kuzingatia kuwa maandalizi yote yameshakamilika kwa kiwango kikubwa na
sisi kama wadhamini wakuu tunahakikisha kuwa mwaka huu kila atakaefika
kwenye ukumbi wa Ubungo Plaza atakuwa na jambo la kusimulia kwa sababu
ni shindano la kipekee.
Shindano hili la Redds Miss Tanzania 2012 linadhaminiwa na Redds Original,Star TV,Giraffe Hotel.
No comments:
Post a Comment