Mkuu wa Wilaya ya Magu, Jaqueline Liana akikata utepe kwenye jiwe la msingi wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji uliogharimu kiasi cha zaidi ya shilingi million 5 katika Kijiji cha Bugabu Wilayani humo.
Mkuu wa Wilaya ya Magu, Jaqueline Liana akifungulia bomba la maji mara baada ya uzinduzi wa mradi wa maji uliogharimu kiasi cha zaidi ya shilingi million 5 katika Kijiji cha Bugabu Wilayani humo.
Mkuu wa Wilaya ya Magu, Jaqueline Liana akimtwisha ndoo ya maji hayo mmoja wa wanakijiji cha Bugabu Wilayani humo.
Mkuu
wa Wilaya ya Magu, Jaqueline Liana amempa saa 24 Mkuu wa Idara ya Maji
wa wilaya hiyo kuwasilisha ripoti ya mradi wa maji uliojengwa katika
Kijiji cha Bugabu uliofadhiriwa na kampuni ya Alpha Choice ya Mwanza.
Amri
hiyo ya Liana inatokana na malalamiko ya wananchi wa kijiji cha Bugabu
wakati wa uzinduzi wa mradi huo wa maji uliogharimu kiasi cha zaidi ya
shilingi million 5.
Akizungumza muda mfupi baada ya kuzindua mradi huo wa maji utakaosaidia
wananchi wa vijiji vitatu, Jaqueline Liana amesema kumekuwa na tabia kwa
wakuu wa idara na viongozi wa vijiji kutosoma mapato na matumizi ya
miradi.
Amesema
kuwepo kwa usiri katika miradi mbalimbali kunawafanya wananchi
kuichukua serikali yao,kitu ambacho kinaweza kuepukwa iwapo suala la
kusomwa mapato na matumizi litazingatiwa.
Afisa
mtendaji wa kijiji cha Bugabu Rebecca Jonas na baadhi ya wananchi wa
kijiji hicho wamezungumzia changamoto mbalimbali kuhusiana na mradi huo
wa maji
Meneja mauzo wa Kampuni ya Alpha Choice inayomiliki viwanda vya
kusindika minofu ya samaki katika nchi za Afrika Mashariki Bruno Mhoja
amesema mradi huo wa maji ni makakati wa kampuni kushirikiana na jamii
katika miradi ya maendeleo.
Mradi huo wa maji ni wa kwanza katika kijiji cha Bugabu kutolewa na wawekezaji ambao utawanufaisha wananchi zaidi ya laki moja.
No comments:
Post a Comment