HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, October 27, 2012

Redd's Miss Talent 2012 ndani ya Giraffe Hotel usiku huu

 Mshindi wa Redd's Miss Talent 2012,Babylove Kalala (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na warembo wengine walioingia hatua ya tano bora ya Redd's Talent iliyofanyika usiku huu katika hoteli ya Gireffe,jijini Dar es salaam.Kutoka kulia ni Mshiriki namba 13 kutoka kanda ya Mashariki,Joyce Baluhi,Mshiriki namba 15 kutoka Temeke,Catherine Masumbigana,Mshiriki kutoka Kanda ya Mashariki,Irene Verda na Mshiriki namba 26 kutoka Kinondoni,Brigit Alfred.
 Mgeni Rasmi katika Onyesho la Redd's Miss Talent,Mbunge wa Viti Maalum - Arusha,Mh. Catherine Magige (katikati) akizungumza machache wakati akifungua shoo hiyo iliyofanyika hivi sasa katika Hoteli ya Giraffe,Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Mkurugenzi wa Rino International Agency ambao ni waandaaji wa Mashindano ya Miss Tanzania,Hashim Lundenga na Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Hoteli ya Giraffe,Dk. Charles Bekon.
 Mshiriki namba 30,Waridi Frank akionyesha umahiri wake wa kucheza ngoma za asili.
 Mshindi wa Redd's Miss Talent 2012,Babylove Kalala akionyesha umahiri wake wa kucheza ngoma za asili kwa kutimia Nyoka.
 Mshiriki namba 11 kutoka Kilimanjaro,Nandi Rafael akionyesha umahiri wake wa kusakata dansi.
 Mshiriki namba 29,kutoka Dodoma,Belinda Mbogo nae akisakata Dansi.
 Mshiriki namba 3 kutoka Chuo Kikuu Huria,Zuwena Naseeb akionyesha umahiri wake wa kuimba katika onyesho la kumpata mrembo mwenye kipaji lililofanyika katika Hoteli ya Giraffe,Mbezi Beach Jijini Dar es Salaam usiku huu.
 Mshiriki namba 13kutoka kanda ya Mashariki,Joyce Baluhi akionyesha uwezo wake wa kusakata dansi.
 Mshiriki namba 27 kutoka Ilala,Noela Michael akionyesha kipaji chake cha kuimba.
 Mshiriki namba 8 kutoka Kanda ya Ziwa,Happyness Rweyemamu akionyesha kipaji chake cha kuruka sarakasi katika onyesho la kumpata mrembo mwenye kipaji lililofanyika katika Hoteli ya Giraffe,Mbezi Beach Jijini Dar es Salaam usiku huu.
 Mshiriki namba 15 kutoka Temeke,Catherine Masumbigana akionyesha kipaji chake cha kupiga Zeze.
Mshiriki namba 7 kutoka Rukwa,Vency Edward akionyesha kipaji alichonacho cha kucheza.


1 comment:

Post Bottom Ad