Profesa wa Taasisi ya Kimataifa ya masuala ya Afya ya
Karolinska Institutet Chini ya taasisi ya World Lung Foundations Staffan
Bergstrom M.D., Ph.D, akionyesha kiwango cha ongezeko la huduma za afya kwa
mama wajawaziti na punguzo la idadi ya vifo, mbele ya waandishi wa habari wakati wa
kutangaza kupatikana kwa mfadhili mwengine wa mradi wa huo jijini Dar es Salaam leo ambao unalengo la kupunguza vifo vya kina mama wajawazito. Awali ufadhili wa
mradi huo ulikua unatolewa na Bloomberg Philanthropies kwa kushirikiana na
Wizara ya afya lakini mfadhili mpya H&B Agerup Foundation ambae amesaini
mkataba jana Jijini Newyork na kushuhudiwa na Rais Kikwete Ban Ki Moon Katibu
Mkuu wa Umoja wa Mataifa, ambapo inakadiriwa zaidi ya kinamama 50,000 hadi 2016
watafaidika.
Mganga Mfawidhi wa kituo Cha Afya Kibiti akieleza mbele ya
waandishi wa habari namna mradi huo ulivyokua na mafanikio kwenye eneo hilo,
ambapo amedai umesababisha hata baadhi ya watu wanaoshi jijini Dar es Salaam
kufuata huduma zao kutokana na mafanikio ya mradi huo. Mradi huu ni wa maeneo
yote muhimu kwa Afya ya mama mjamzito kuanzia vifaa wataalamu na hata
miundombinu ya Hospitali.
Naibu Mkurugenzi wa Mradi ambaye ni Daktari bingwa wa
upasuaji Dk. Hemed Mahfudh akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali kwa wandishi
wa habari mara baada ya mkutano.
No comments:
Post a Comment