Siku
ya Jumamosi tarehe 27.10.12 Mh Balozi wetu wa Tanzania nchini
Uingereza,Mh. Peter Kallaghe alishiriki sherehe ya siku kuu ya Iddi
iliyofanyika London mashariki.
Sherehe
hii ya baraza la EID (IDDI) iliyoandaliwa na Jumuiya ya East African
Education Foundation wakishirikiana na Jumuiya ya Wazanzibari waishio UK
(ZAWA).
Wakati
akitoa hotuba yake Mh Balozi Peter Kallaghe ambaye ndio aliekua mgeni
rasmi siku hiyo, alianza kwa kuwashukuru kwa mualiko huo mzuri alioupata
na kuwatakia kila kheri wale wote waliofanikiwa kutekeleza HIJA kwa
mwaka huu 2012.
Aidha
Mh Balozi aliahidi kuendeleza ushirikiano uliopo baina ya Ubalozi na
Jumuiya mbalimbali za Watanzania zilizopo nchini Uingereza na Ireland.
Pia
alivutiwa na kuipongeza hatma ya East African Education Foundation
kuazimia kununua Jengo kwa ajili ya shughuli za kijamii na wanajumuiya
wote kwa ujumla.
Baada ya kumaliza hotuba yake Shekhe Nasssor Haroub nae aliongea na
wanajumuiya akitilia mkazo zaidi umuhimu wa Umoja na mshikamano kama
Uislamu unavyo sisitiza kupitia Ibada ya HIJA.
Vilevile
vijana wa kasida walipata fursa ya kutumbuiza alipomaliza kuongea
Shekhe Nassor.
Mwishoni Balozi alifanya ziara fupi ya kukagua jengo la Jumuiya hiyo na
kupata maelezo kutoka kwa viongozi mbalimbali wa Jumuiya ili kujua
namna gani litakavyoweza kutumika mara baada ya hatua za ununuzi
zitakapo kamilika rasmi kwa gharama za paundi laki 6 (£600,000)
Asanteni,
Urban Pulse Creative
Mh Balozi katika akipokea zawadi kutoka kwa wanajumuiya
Mh. Balozi Peter Kallaghe akiwa katika Picha ya pamoja na Wanajumuiya ya East African Education Foundation.
Mwenyekiti wa ZAWA,Hassan Khamis akimfafanulia jambo Mh Balozi.
Ustadhi akiongea machache wakati wa chakula.
Vijana wa Kasida wakitumbuiza.
watoto wa Kasida wakisikiliza Hotuba ya Mh Balozi.
No comments:
Post a Comment