HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, October 22, 2012

MASHINDANO YA MITUMBWI YA BALIMI MJINI KIGOMA


Timu ya katonga A ambao ni mabingwa wa mkoa wa Kigoma wakimaliza mashindano ya kupiga makasia ya Bia ya Balimi kwenye Ziwa Tanganyika.
Meneja wa Bia ya Balimi Edith Bebwa kulia akishuhudia namna wachezaji wa timu mbalimbali walivyokuwa wakitoana jasho kwenye fainali ya Mashindano ya Kupiga makasia ya Bia ya Balimi kwenye ziwa Tanganyika.
Mabingwa wa mashindano ya Balimi boat race mkoa wa kigoma upande wa wanaume Timu ya Katonga A wanaume wakishangilia mara baada ya kuwa mabingwa wa mkoa huo na kukabidhiwa jumla ya shilingi laki tisa kama zawadi ya ushindi wa kwanza.
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Mh Ramadhani Maneno akimkabidhi kitita cha Shilingi laki saba kepteni wa timu ya wanawake ya upendo bi mawazo shaban Juhudi mara baada ya kuibuka kidedea kwenye fainali hiyo. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad