Meneja
Masoko wa Kampuni ya Megatrade Investment Limited,Bw. Goodluck Kway
(kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi Milioni
10,Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Jambo Festival ambaye pia ni
Afisa Mkuu Mtendaji wa Idea Afrika ambao ndio waandaaji wa tamasha
hilo,Bw.Augustine Namfua kwaajili ya kudhamini Tamasha la Jambo Festival
linalotarajiwa kufanyika Oktoba 20 hadi 28 mwaka huu jijini Arusha.
Na Woinde Shizza,Arusha
KAMPUNI
ya Mega trade Investment kupitia kinywaji chake cha K -Vant Gin
wamekabithi kiasi cha hundi ya shs 10 milioni kwa ajili ya kudhamini
tamasha la kimataifa la Arusha la sanaa na utamaduni (Jambo Festival
litakalofanyika oktoba 20 hadi 28 mwaka huu mkoani Arusha.
Akizungumza wakati wa kukabithi hundi hiyo ,Meneja masoko wa Megatrade
,Goodluck Kway alisema kuwa tamasha hilo litahusisha wapenzi wa sanaa za
mikono,maonyesho, ubunifu na utamaduni kutoka maeneo mbalimbali ndani
na nje ya nchi.
Kway
alisema kuwa, baadhi ya faida nyingi zitakazopatikana kupitia tamasha
hilo ni pamoja na kupandisha hadhi ya jiji la Arusha na kuliweka katika
sura mpya na bora zaidi katika ramani ya ulimwengu , kuvutia na kukuza
na kuendeleza utalii wa kawaida wa ndani na nje ya nchi.
Alisema
kuwa,tamasha hilo litawezesha kutengeneza nafasi za ajira na biashara
kwa vijana, wanawake na wafanyabiashara kwa ujumla kabla, wakati na
baada ya tamasha, kutoa nafasi kwa wajasiriamali na wafanyabiashara
kushiriki na kufanya biashara katika tamasha hili na maonesho haya,
kukuza na kuendeleza utalii wa kitamaduni lakini pia kutoa fursa adimu
kwa jamii za Arusha na watanzania kwa ujumla kusherehekea sanaa na
utamaduni wao wa asili.
Kway alisema kuwa, tamasha la Jambo linatarajiwa kuchukua takribani siku tisa likijumuisha shughuli na matukio mbalimbali.
Naye
Afisa Mkuu wa kampuni ya Idea Afrika ambao ndio waandaji wa tamasha
hilo, ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya tamasha
hilo,Augustine Michael Namfua alisema kuwa,amefurahishwa sana na msaada
huo kutoka Mega kwani ndio wadhamini wakuu.
Namfua
alisema kuwa,fedha hizo watazitumia kwa umakini uliokusudiwa katika
kuhakikisha wamewasadia vijana mbalimbali katika kuibua vipaji vyao na
hatimaye tamasha hilo kuwa la mafanikio makubwa.
Aliwataka
vijana kujitokeza kwa wingi kuja kuinua vipaji vyao katika tamasha hilo
kwani hiyo ndiyo fursa pekee ya kuweza kujifunza kupitia kwa wasanii
wenzao
No comments:
Post a Comment