Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando (kushoto) akiongea wakati wa uzinduzi wa ushirikiano wa kampuni ya simu za Mkononi ya Airtel na Bank of Afrika katika kutoa huduma ya Airtel money kupitia matawi ya bank hiyo yote yaliyopo Tanzania. Uzinduzi huo ulifanyika jana katika Makao makuu ya Airtel Morocco Jijini Dar es Salaam. pichani kulia ni mkuu wa kitengo cha IT Bank of Afrika bwn. Willington Munyanga , akifatiwa na Mkuu wa huduma za kibenki Mwanahiba Mzee na anayefatia ni Meneja Airtel Money John Ndunguru.
Meneja Airtel Money John Ndunguru na Mkuu wa huduma za kibenki Mwanahiba Mzee kwa pamoja wakikabidhiana mikataba mara baada ya makubaliano ya ushirikiano wa Airtel na Bank of Afrika katika kutoa huduma ya Airtel money kupitia matawi ya bank hiyo yote yaliyopo Tanzania. Makabidhiano hayo yalifanyika jana katika Makao makuu ya Airtel Morocco Jijini Dar es Salaam. wakishuhudia Katikati ni Mmoja ya wakala mkubwa wa Airtel money kutoka kampuni ya Connexions bwn Shyamkumar Balakrishnan (katika) na kushoto ni Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando.
Meneja Airtel Money John Ndunguru na Mkuu wa huduma za kibenki Mwanahiba Mzee wakipitia mkataba mara baada ya makubaliano ya ushirikiano wa Airtel na Bank of Afrika katika kutoa huduma ya Airtel money kupitia matawi ya bank hiyo yote yaliyopo Tanzania.
No comments:
Post a Comment