HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, September 27, 2012

Wadau tumshauri nini huyu Dada??


Dear Mdau,

Nategemea barua hii itakukuta salama. Mimi ni msichana wa miaka 23. Nilifiwa na wazazi wangu wakati nikiwa na miaka minane. Bibi yangu alishindwa kunilipia shule hivyo nikawa nyumbani tu, bahati nzuri mvulana mmoja kijijini kwetu akanambia atanisaidia, wakati huo alikuwa anauza machungwa barabarani.


 Kweli alianza kunilipia shule, miaka yote, hatimae hata yeye akabadili kazi akaanza kuendesha daladala, na ameendelea kunilipia mpaka sasa niko chuo kikuu. Namshukuru Mungu kwa kunikutanisha na malaika kama huyu sijui siku hizi ningekuwa wapi.


Tatizo langu ni kuwa anataka kunioa nikimaliza chuo, na mimi kwa kweli nashindwa kumwambia kuwa itakuwa vigumu kwa kuwa yeye siyo 'type' yangu. Hebu fikiria mimi ni graduate halafu naolewa na dreva wa daladala, ni wazi kuwa si type yangu. 


Ninachoomba ni busara zako ntamwambiaje bila kumuumiza, kuwa haiwezekanai mimi nikaolewa na yeye?

Chanzo : Kitime Blog.

8 comments:

  1. kweli shukrani ya Punda mateke, yaani yote umesahau aliyokufadhili mwisho wake ndio huo baada ya kufika chuo kikuu unasema jamaa sio type yako.endelea kuwa na fikra hizo za kuwa jamaa hakufai,ipo siku itafika na utampata aliyekuwa type yako lakini hutapata mapenzi kama ya jamaa muuza machungwa.
    Mwenyezi mungu atamlipia jamaa fadhila zake alizotoa kwako,elewa mtenda hutendwa. kwa ushauri wangu ikiwa ni mimi sikuoi kwani tayari umeshaanza kuleta dharau hata kabla hujaolewa je ukishaolewa itakuwaje? utajiona wewe ni high class na mimi kwa kuwa sina elimu ni low class na sio type yako. Na hata kama utakubali kuolewa ni kazi bure, Dharau na masimango havitakwisha ndani ya nyumba. mapenzi kwa mumeo hayatakuwepo.

    ReplyDelete
  2. Yani nilipomaliza kusoma hii habari nimejikuta natukana bila kutegemea, yani huyo dada hana akili hata kidogo pamoja na kwamba mimi ni mwanamke kama yeye, hivi kwa akili za kibinadamu unaweza kujiuliza mara mbili kweli??? au akili zake haziko sawa?? Wema wote huo haoni? Kama kweli umesoma na uko chuo kikuu basi hata unachokisoma hukielewi, unashindwa kufikiri ukimaliza chuo upate kazi kwa nini usitafute hata mradi ukamtoa huyo kaka wa watu kwenye hiyo kazi iliyofanya wewe kufika hapo mpaka leo kufikiria kuwa na jeuri ya kuona yeye sio type yako akasimamia mradi wenu mkaendesha maisha yenu huna haya hata kidogo. Na Laana ya Mungu iko karibu yako. Hao wanao kuona wa maana sasa hivi ni kwa ajili ya huyo huyo dereva dala dala wa watu aliye jitoa kwa hali na mali mpaka wewe kufika hapo. Shame on u

    ReplyDelete
  3. Kwanza huyo binti abadilishe kauli kuwa si type yake sababu eti yeye ni msomi na mwenzie ni muendesha daladala, ajiulize bila hiyo kazi ya daladala yeye angekuwa wapi sasa hivi? Akumbuke pia kuna Mungu kwa nini hakumkutanisha na msomi na kumpa msaada mkubwa kama huo? Atoe sababu nyingine ila kwa hiyo aliyoieleza hapo inaonesha wazi kuwa ana elimu lakini hajaelimika. Nasikitika kuwa mpaka leo kuna watu wanalinganisha mapenzi na elimu zao, pesa zao, umaarufu nk. Mimi nadhani hajampenda na wala si kazi alitonayo huyo kijana.

    ReplyDelete
  4. KWA KWELI MIMI BINAFSI SIMUELEWI KABISA HUYU DADA. MTU AMEMUHUDUMIA MIAKA YOTE HIYO, LEO HII ANASEMA SIYO TYPE YAKE!!! KWANI HUYO KIJANA SI NDO AMEMTOA KWENYE TYPE YA KUUZA VITUMBUA MBELE YA DUKA LA KIJIJI??? IWEJE LEO AMDHARAU. HIVI ANAFAHAMU MAISHA YA HUYO KIJANA AMEYAWEKEZA KWA HUYU DADA?? AMEPOTEZA PESA ZAKE KIBAO, AMEMSUBIRI MUDA MREFU KWA KUACHA KUOA WASICHANA WENGINE, KUMBE HATHAMINIWI. HUYU DADA AKIMWACHA AKAOLEWA NA MWINGINE ANAYEMWITA WA TYPE YAKE, ASUBIRI KISASI TOKA KWA MUNGU. KWANI APANDACHO MTU NDICHO ATAKACHO VUNA!!!!!! MASIKINI HUYO KAKA ANAWEZA HASIOE KABISA KWA KUOGOPA KUWA WANAWAKE WOTE NDIVYO WALIVYO.

    ReplyDelete
  5. Huyo Dada ni mjinga wala asijidanganye eti amesoma bado kaujinga kapo.Bila huyo muendesha daladala hayo mashauzi angeyatoa wapi? tena ataolewa na Kichaa wa Mji. Hii dunia sio0 ya kuiga kaa tafakali upate jibu Kamili,acha kupaparuka wala hauna ulilolisoma kuna watu wana PHDlakini wanaolewa na wanaume ambao hajasoma na wanaishi maisha mazuri wewe ako ka STASHAHADA ndo kanakudanganya.Tulia na huyo Mungu aliye kuchagulia.

    ReplyDelete
  6. sas amekuwa siyo type yako vp kwani huyo kijana amekuokota na kukusaidia hao type yako walikuwa wapi kukusaidia? ninakushauri kitu kimoja sijui huko bongo ila wenzetu wazungu hawajali sana type ya mtu ila as man bringing the bread on the table is the main thing na maelewano, nafikiri umenipata. utawafata hao type yako wakakurusha roho mpaka utatia akili huyo jamaa anaweza akawa ndioyo nyota yako kwani kaweza kukusomesha mpaka chuo kikuu wakati elimu yake ndogo soyo mcheto.pima!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  7. wewe msichana mpumbavu yaani unamwacha mwenzako kwa sababu umesoma kama je ni wewe ungekuwa dereva wa daladala halafu anasema akuache ungefurahi?
    Nashauri Kwanza tutangazie Arusi,huyu mtu wa size yako,umetoka naye mbali huyo ndiye anaye kufaa.USIMWACHE NAKUSHAURI,au jaribu halafu utasimulia matokeo baadaye.

    ReplyDelete
  8. kweli wewe mwanamke huna shukurani wsala imani

    ReplyDelete

Post Bottom Ad