Meneja
wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo akizungumza na wachezaji wa
Pool (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa mashindano ya Safari Pool
Taifa yaliyofunguliwa rasmi na Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Amina Masenza
katika Hoteli ya Monarch jijini Mwanza jana.
Mkuu
wa Wilaya ya Ilemela, Amina Masenza akizungumza na wachezaji (hawapo
pichani) wakati wa ufunguzi wa mashindano ya Safari Pool Taifa katika
Hoteli ya Monarch jijini Mwanza.Kushoto ni Meneja wa Bia ya Safari
Lager, Oscar Shelukindo na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Pool Taifa,
Fred Mushi.
Mkuu
wa Wilaya ya Ilemela, Amina Masenza (wapili kulia) akifungua rasmi
mashindano ya Safari Pool Taifa .Kulia ni Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya
Ilemela(OCD),Debora Magiligimba.Wengine kutoka kushoto ni Katibu wa
chama cha Pool Mkoa wa Ilala, Mohamed Mwarabu, Mwenyekiti wa kamati ya
mashindano, Haji Kapulila na Makamu mwenyekiti wa TAPA, Fred Mushi.
Waamuzi
wa mchezo wa Pool wakiongoza maandamano ya kuingia ukumbini wakati wa
ufunguzi wa mashindano ya Safari Pool Taifa yaliyofunguliwa rasmi jana
katika Hoteli ya Monarch jijini Mwanza na Mkuu wa Wilya ya Ilemela,
Amina Masenza.
Na Mwandishi Wetu,Mwanza
MKUU wa Wilaya ya Ilemela mkoa wa Mwanza, Amina Masenza amewataka viongozi wa vyama
vya mchezo wa pool kuanzia Wilaya, Mikoa na Taifa kuwapa nafasi
wachezaji wanawake ili kuweza kuwajengea uwezo wa kujiamini wa kucheza
mchezo huo.
Masenza
aliyasema hayo jana wakati alipokuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa
fainali za taifa za mashindano ya 'Safari Lager National Pool
Championship 2012', kwenye ukumbi wa hoteli ya Monarch mkoani hapa.
Alisema kuwa kama viongozi wa vyama vya mchezo huo kuanzia wilaya hadi taifa watatoa
kipaumbele kwa wachezaji wanawake katika kucheza mchezo huo itawasaidia
zaidi katika kuwajengea uwezo wa kujiamini na pia itakuwa ni changamoto
kwa wanawake wengine kujitokeza.
"Mwanamke
akiwezeshwa anaweza, hivyo toeni kipaumbele kwa wachezaji wanawake ili
kuweza kuwajengea uwezo wa kujiamini katika kucheza na pia iwe
changamoto kwa wanawake wengine kujitokeza zaidi katika kucheza mchezo
huu"alisema Masenza.
Aliongeza
kwa kuwataka waamuziwatakaochezesha fainali hizo kuchezesha kwa haki
ili kuepukana na vurugu zinazoweza kutokea kutokana na uamuzi wa
upendeleo.
Masenza alisema kuwa waamuzi kama watachezesha kwa haki ana imani fainali hizo zitamalizika bila vurugu zozote.
"Niwaombe
waamuzi chezesheni kwa haki ili kuepuka vurugu ambazo zinaweza kutokea
kutokana na maamuzi ambayo siyo mazuri,"alisema.
Aidha amewataka viongozi, wachezaji na mashabiki kuwa na imani na viongozi wao wa taifa wa mchezo huo na kuepuka maneno ya pembeni ambayo yanaweza kupelekea vurugu sizokuwa na msingi.
Masenza
aliwapongeza wadhamini wakuu wa mchezo huo nchini, Kampuni ya Bia
Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager kwa kuweza kuinua na
kuukuza mchezo huo.
Naye
meneja wa bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo alisema kuwa
wataendelea kudhamini mchezo huo lengo likiwa ni kuuendeleza na kutoa
mchango wao katika jamii kwa faida wanayoipata kupitia kwenye bia yao.
"Nia
ya kuanza kudhamini mchezo wa pool ilikuwa ni kuinua na kuukuza, hivyo
tutaendelea kuudhamini huku tukiwa tunatoa pia mchango wetu katika jamii
katika faida kidogo tunayopata kupitia kiwenye bbia bia yetu ya Safari
Lager,"alisema Shelukindo.
Mkuu wa wilaya ya kipolisi ya Ilemela (OCD),Debora Magiligimba amewataka viongozi, wachezaji na mashabiki wa timu zote za mikoa 16 inayoshiriki fainali hizo kuishi kwa amani katika siku zote za mashindano hayo kutokana na kwamba ulinzi utaimalishwa na atakayesababisha vurugu atashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.
Timu
zinazoshiriki fainali hizo na mikoa zinakotoka ikiwa kwenye mabano ni
Spider (Tanga), Janja (Manyara), New Stand (Shinyanga), Texas (Tabora),
Sabasaba (Lindi), Anatory (Morogoro), Atlantic (Dodoma), Nginja (Iringa)
na Blue House (Mbeya).
Nyingine
ni Bilele (Kagera), Meeda (Kinondoni), Mbosho (Kilimanjaro), 2eyes
(Arusha),Kayumba (Ilala), Sun City (Temeke) na wenyeji Paseansi
(Mwanza).
Bingwa
wa taifa wa fainali hizo kwa upande wa klabu ataondoka na Sh.Mil.5,
wakati ambapo bingwa kwa upande wa mchezaji mmoja mmoja (wanaume)
atazawadiwa Sh.500,000 na kwa upande wa wanawake bingwa atajizolea
Sh.350,000.

No comments:
Post a Comment