HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, September 2, 2012

TIMU YA JAMHURI YANYAKUA NGAO YA HISANI ZANZIBAR

 Mgeni Rasmi katika Mchezo wa Kombe la Hisani kwa ligi kuu ya Grand Malt Zanzibar,Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii (SMZ),Mh. Juma Hajji Duni (kushoto) akikabidhi Ngao hiyo kwa Nahodha wa Timu ya Jamhuri kutoka kisiwani Pemba,Ally Said Choma baada ya kuinyuka mabao timu ya Super Falcon mabao 3-1 katika mchezo uliopigwa jana usiku kwenye uwanja wa Amani,Zanzibar.Katikati ni Meneja Masoko wa Grand Malt,Fimbo Butallah.
 Nahodha wa timu ya Jamhuri,Ally Said Choma akinyanyua Ngao ya Hisani juu baada ya kukabidhiwa na mgeni rasmi,Mh. Hajji Duni (wa tatu kulia).wengine pichani ni toka kushoto ni Meneja wa kinywaji cha Grand Malt,Consolata Adam,Makau wa Rais wa ZFA,Kassum Suleman,Waziri wa Mifugo na Uvuvi (SMZ),Mh. Abdillahi Jihadi Hassan na Meneja Masoko wa Grand Malt,Fimbo Butallah.
Picha ya Pamoja na Mabingwa wa Ngao ya Hisani Zanzibar 2012.
Furaha ya kunyakua Ngao ya Hisani ilitawala kwa Wachezaji wa Timu ya Jamhuri.
Mpira umekwishaaaaaa...... na matokeo ndio yaleee ubaoni.
Beki wa Timu ya Super Falcon,Faki Ali (3) akiwahi kuuzuia mpira uliokuwa ukielekea kwa mshambuliaji wa timu ya Jamhuri,Ally Said Choma (9) wakati wa mchezo wa ngao ya hisani yenye kuashiria uzinduzi rasmi wa ligi kuu ya Grand Malt Zanzibar 2012 uliochezwa kwenye uwanja wa Amani,Zanzibar.Timu ya Jamhuri ndio iliibuka kidedea kwa kuwalaza wenzao wa Super Falcon mabao 3-1.
Chumaaaaa.....
Mshambuliaji wa timu ya Super Falcon,Hemed Bakari (9) akijaribu kumzungusha Beki wa timu ya Jamhuri,Mulid Othman wakati wa Mchezo wao wa kuwania Ngao ya Hisani uliofanyika jana usiku kwenye uwanja wa Amani,Zanzibar.
heka heka uwanjani.
hapiti mtu hapa.
Mgeni rasmi akikagua timu na kusalimia na wachezaji.
Meneja wa Kinywaji cha Grand Malt ambao ndio wadhamini wa ligi kuu ya Zanzibar,Consolata Adam akipeana mkono na wachezaji kabla ya mtanange kuanza akifuatiwa na Meneja Mauzo,Bw. Tarimo.
Maandamano ya Ufunguzi wa Ligi kuu ya Grand Malt Zanzibar yakipita jukwaa kuu.
Timu mbali mbali zikiwa na mabango yao uwanjani.
Vijana wakionyesha umahiri wao wa kuchezea mpira.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad