HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, September 2, 2012

Mh. Lowasa apigania haki ya wafugaji kikatiba

Waziri Mkuu mstaafu ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jamii ya Kimasai Afrika Mashariki, Mh. Edward Lowassa akizungumza katika mkutano wa viongozi wa jamii ya kimasai jana kwenye mjini Monduli Mkoani Arusha.
Baadhi ya viongozi wa kimila wa jamii ya kimasai wakifuatilia mkutano wa viongozi unaoendelea mjini Monduli Mkoani Arusha.
Waziri Mkuu mstaafu,Mh. Edward Lowassa akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Sokoine Morogoro,(kushoto) ni Sarah Motosyo Kalaita na kulia ni Kamando Nambalo, wanafunzi hao wanatoka katika jamii ya wafugaji wa kimasai.
 
 Na Mwandishi Wetu.
 
JAMII ya Wafugaji wamemwomba Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa kuwasidia iliwatambuliwe katika katiba mpya kiasi kwamba waweze kupata haki ya kumiliki ardhi.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika mkutano wa viongozi wa kimila wa jamii ya kimasai iliyofanyika jana mjini Monduli Mkoani Arusha walisema kwamba wafugaji wanapata shida kwasababu hawatambuliki kikatiba.
William Ole Seki ambaye ni Katibu wa Mbunge wa Ngorongoro Saning’o Ole Telele alisema “wafugaji wanakatazwa kulisha mifugo katika misitu, kwa madai kwamba ni maeneo ya wakulima, wanakatazwa kunywesha mifugo yao katika mabwawa na mito ya maji bila kujali kwamba mifugo ndiyo njia kuu ya uchumi ya wafugaji”.
Mwenyekiti wa viongozi wa mila wa jamii ya Kimaasai amesema wafugaji nchini watadai haki ya kutambuliwa na katiba mpya na wanakusudia kujifunza kutoka kwa wenzao wa nchi jirani ya Kenya walivyofanikisha hilo.
 
Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowassa akizungumza kakati ufunguzi wa kikao hicho alisema kwamba imefika wakati ambapo jamii ya wafugaji watambuliwe katika katiba mpya.
Alisema kwamba jamii ya wafugaji wakitambuliwa katika katiba mpya itawapa mwanya wakumiliki ardhi na kutokomeza migogoro mbalimbali inayojitokeza kati ya wakulima na wafugaji.
 
“Wafugaji wanapaswa kutambuliwa kikatiba ili wapate haki ya kumiliki ardhi kwani wafugaji wanategemea mifugo yao kama njia kuu ya uchumi na ili mifugo hiyo iweze kuzaliana kwa wingi na kuwanufaisha wafugaji,ni lazima wawe na ardhi”alisema Lowassa na kungeza:
 
“Ili mfugaji aweze kunufaika na mifugo yake lazima apate ardhi itakayomwezesha kutunza mifugo yake, kwani mifugo inahitaji maji na malisho, sasa kama mfugaji huyu hatambuliki kikatiba na kupewa haki ya kumiliki ardhi hawezi kuwa na nguvu yakufuga mifugo na kujikwamua kiuchumi”.
 
Alisema kwamba mifugo ndiyo njia kuu ya uchumi na kipato cha mfugaji hivyo lazima katiba mpya iwatambue na wapate haki yao kikatiba kama wafugaji halisi ndani ya nchi kama ilivyo kwa nchi za wenzetu hususan nchi jirani ya Kenya.
 
“Ili kufanikisha hili tutajitahidi kujifunza namna ambavyo wenzetu wa Kenya walivyofanikisha suala hili na kuliingiza katika katiba mpya ya nchi hiyo, ikibidi kwenda Kenya tutakwenda kujifunza juu ya hili”alifafanua Lowasa.
 
Mkutano huo wa siku mbili ulihudhuriwa na watu wapatao 150 kutoka mikoa ya Arusha, Morogoro na Mbeya.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad