Saturday, July 21, 2012

SALAAM ZA RAMBIRAMBI KUTOKA JAPAN KUFUATIA AJALI YA MELI ZANZIBAR

Kwa niaba ya Jumuiya ya Watanzania, na Watanzania wote tunaoishi nchini Japan naomba niwajulishe kwamba tumepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya ajali ya meli ya MV SKAGIT,iliyokuwa ikisafiri kutoka Dar kuelekea Zanzibar, ambayo imesababisha wenzetu wengi kupoteza maisha na wengine kujeruhiwa.


Tunawapongeza na kuwashukuru taasisi mbali-mbali na watu binafsi wanaofanya kazi kubwa kukabili zoezi la uokoaji, na wale waliotufikishia habari hizi. Tunawashukuru wale wote waliopata taarifa na kuelekea kwenye eneo la tukio na kuanza uokoaji mara moja.


Uongozi wa Jumuiya ya Watanzania, na Watanzania wote tunaoishi nchini Japan, tuko pamoja nanyi,na pia tunaungana na Watanzania wenzetu wote kutoa pole kwa wafiwa, na kuwaombea majeruhi waweze kupona kwa haraka. 


Tunamuomba Mwenyezi Mungu aziweke pema peponi roho za marehemu wote nakuwapa nguvu na uvumulivu ndugu na jamaa, katika kipindi hiki kigumu.


NJENGA, Rashid
Mwenyekiti,
Jumuiya ya Watanzania Waishio nchini Japan.

No comments:

Post a Comment