Friday, July 20, 2012

Yanga yaonyesha kandanda la ukweli uwanja wa Taifa jijini Dar leo,Yaichapa APR ya RWANDA bao 2-0

 Beki wa Timu ya APR,Mbuyu Twite akimzuia Mshambuliaji machachari wa timu ya Yanga,Said Bahanuz ili asiuchukue mpira kwenye mchezo unaoendelea hivi sasa katika uwanja wa Taifa jijini Dar.Yanga imeitungua APR bao 2-0.
 Jerry Tegete akiwania mpira na Beki wa APR.
 Mashabiki wa timu ta Yanga wakiishangilia timu yao baada ya kupata ushindi dhidi ya timu ya APR ya Rwanda katika mchezo uliopigwa jioni hii katika uwanja wa Taifa jijini Dar ikiwa ni muendelezo wa Mashindano ya Kombe la Cecafa Kagame.Yanga imeshinda bao 2-0.
 heka heka langoni mwa APR.


 Wachezaji wa Yanga wakishangilia bao lao la kuongoza lililofungwa na Said Bahanuz dakika ya 28 ya mchezo kipindi cha kwanza,huku mwamuzi wa mchezo huo akiwataka kurudi uwanjani.

 Nizar Khalfan wa Yanga akiwachambua mabeki wa APR.


No comments:

Post a Comment