HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, July 27, 2012

MADIWANI WA ILALA WAPITISHA SHERIA YA HUDUMA YA MFUKO WA BIMA YA AFYA NHIF KATIKA MANISPAA HIYO

Meya wa Manispaa ya Ilala,Mh. Jerry Silaa akiongoza kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika kwenye ukumbi wa Anatouglo jijini Dar es salaam, kazi kubwa ya Baraza jilo la Madiwani ilikuwa ni kupitisha sheria ya Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) ambapo sasa mfuko huo kupitia TIKA utaanza kutoa huduma za matibabu kwa wakazi wa manispaa hiyo ili kupunguza gharama za matibabu kwa wananchi wa manispaa hiyo hasa wale wenye kipato cha chini.
Mmoja wa watumishi wa Manispaa hiyo akitoa SIWA mara baada ya Baraza hilo la madiwani kupitisha sheria hiyo na kuahirisha kikao hicho.

Madiwani mbalimbali wakiwa katika kikao hicho cha Baraza la Madiwani.
Madiwani wakiwa wamesimama baada ya kumalizika kwa kikao.
Meya wa Manispaa ya Ilala akiwa katika picha ya pamoja na Wakuuwa Mfuko wa Bima ya Afya NHIF baada ya kumalizika kwa kikao hicho cha madiwani.
Wakuu wa Mfuko wa Bima ya Afya ya Jamii NHIF wakiwa katika picha ya pamoja.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad