HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, July 4, 2012

KUELEKEA TAMASHA LA MATUMAINI: BONGO FLEVA, BONGO MOVIE WAPIGANA MKWARA

Baadhi ya wachezaji wa Bongo Fleva wakiwa mazoezini.



TIMU za mpira wa miguu za wasanii wa muziki, Bongo Fleva, na wacheza sinema, Bongo Movie, jana zilizidi kutoleana vitisho kwenye mazoezi yaliyozikutanisha katika Viwanja vya Leaders Club Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Timu ya Bongo Movie, Jacob Steven ‘JB’, alisikika akisema kuwa hakuna mechi itakuwa chungu kwa Bongo Fleva kama ya Tamasha la Matumaini itakayofanyika Jumamosi hii, ambapo wanatarajia kuwapakiza mvua ya magoli.

Nao Bongo Fleva, kupitia mchezaji wao Kala Pina, walisema mazoezi wanayoyapata kutoka kwa kocha wao, Seleman Matola, wanawaomba Bongo  Movie wajitoe mapema mechi hiyo kwani moto wake utakuwa mkali isivyo kawaida. (Habari/Picha: Musa Mateja/GPL)
Bongo Fleva wakiwa ‘siriaz’ mazoezini.
Kala Pina (katikati), akipasha misuli na wenzake.
Mchezaji wa Bongo Fleva, Suma G akijinoa.
Amini Mwinyimkuu na wenzake.
JB (wa kwanza kushoto) ‘akijikomaza’.
Vicent Kigosi ‘Ray’ wa Bongo Movie akijiwinda kwa mpambano wa Jumamosi.
Mshambuliaji wa kulia wa ‘Bongo Movie’, Hartman Mbilinyi akipiga shuti wakati wa mazoezi.
Inspector Haroun wa Bongo Fleva akiwa mazoezini.
Mussa Issa ‘Cloud’ wa Bongo Movie (kulia) akiwania mpira na mwenzake.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad