HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, June 25, 2012

WASHINDI WA TUZO ZA EXCEL WITH GRAND MATL MKOA WA KILIMANJARO WAKABIDHIWA ZAWADI ZAO

 Washindi wa Tuzo za Excel With Grand Malt kwa vyuo vya Elimu ya Juu mkoani Kilimanjaro (Chuo cha Ushirika na Chuo cha Kumbukumbu ya Mt. Stefano) wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mgeni Rasmi kwenye utoaji wa Tuzo hizo,Kaimu Katibu Tawala wa Halmashauri ya mji wa Moshi,Bi. Ruth Malisa (wa sita kutoka kulia walio mstari wa nyuma) na Meneja wa kinywaji kisicho na kilevi cha Grand Malt ambao ndio wadhamini wakuu wa Mashindano hayo,Bi. Consolata Adam (katikati waliosimama mstari nyuma) huku wakionyesha zawadi zao walizoshinda wakati wa Sherehe za utoaji wa tuzo hizo zilifanyika kwenye viwanja vya Hindu Mandal,Mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro.
 Mgeni Rasmi kwenye utoaji wa Tuzo za Excel With Grand Malt ,Kaimu Katibu Tawala wa Halmashauri ya mji wa Moshi,Bi. Ruth Malisa (pili Kulia) akikabidhi Cheti cha Shukrani kwa Waziri wa Michezo wa Chuo Kikuu cha Ushirika,Ramadhan Mkambala wakati wa sherehe za Utoaji wa Tuzo hizo,zilifanyika kwenye viwanja vya Hindu Mandal,Mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro.Kushoto ni Meneja wa kinywaji cha Grand Malt ambao ndio wadhamini wakuu wa Mashindano hayo,Bi. Consolata Adam na wapili kulia ni Muwakilishi wa TBL Mkoa wa Kilimanjaro,Edmund Rutaraka.
 Mgeni Rasmi kwenye utoaji wa Tuzo za Excel With Grand Malt ,Kaimu Katibu Tawala wa Halmashauri ya mji wa Moshi,Bi. Ruth Malisa (pili Kulia) akikabidhi Cheti cha Shukrani kwa Waziri Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mt. Stefano,Josephat Bakes wakati wa sherehe za Utoaji wa Tuzo hizo,zilifanyika kwenye viwanja vya Hindu Mandal,Mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro.Kushoto ni Meneja wa kinywaji cha Grand Malt ambao ndio wadhamini wakuu wa Mashindano hayo,Bi. Consolata Adam na wapili kulia ni Muwakilishi wa TBL Mkoa wa Kilimanjaro,Edmund Rutaraka.
 Baadhi ya Washindi mbali mbali wa Tuzo hizo za Excel With Grand Malt wakionyesha fedha zao walizokabidhiwa kwa ushindi wao huo.
 Meneja wa kinywaji cha Grand Malt ambao ndio wadhamini wakuu wa Mashindano hayo,Bi. Consolata Adam akizungumza na washindi pamoja na washiriki mbali mbali wa tuzo hizo.
  Mgeni Rasmi kwenye utoaji wa Tuzo za Excel With Grand Malt ,Kaimu Katibu Tawala wa Halmashauri ya mji wa Moshi,Bi. Ruth Malisa akisisitiza jambo kwa wanachuo hao walioshiriki kwenye tuzo hizo.
Ni furaha kwa kila mshindi.
 Mwanamuziki mkongwe wa Muziki wa Bongo Fleva,Joseph Haule a.k.a Profesa Jay akiwabagawisha mashabiki wake wa mkoani wa Kilimanjaro wakati wa Sherehe za Utoaji wa tuzo za Excel With Grand Malt,zilizofanyika kwenye viwanja vya  Hindu Mandal,mjini Moshi.
 Profesa Jay akimsikiliza kwa makini mdogo wake ambaye alikuwa akiflow ile mbayaaa......
 Burudani zingine zikiendelea.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad