Washindi wa Tuzo za Excel With Grand Malt kwa vyuo vya Elimu ya Juu mkoani Iringa wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mgeni Rasmi kwenye utoaji wa Tuzo hizo,Mkuu wa Wilaya ya Iringa,Mh. Leticia Warioba (wa tatu toka kushoto walio mstari wa mbele) na Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania,Fimbo Butallah (wa nne toka kushoto walio mstari wa mbele) ambao ndio wadhamini wakuu wa Tuzo hizo kupitia kinywaji kisicho na kilevi cha Grand Malt.Wa pili kushoto ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Tumaini,Prof. Enock UgulumuSherehe ya utoaji wa tuzo hizo ilifanyika kwenye viwanja vya Chuo kikuu cha Tumaini,Mkoani Iringa.
Washindi wa Tuzo za Excel With Grand Malt kwa vyuo vya Elimu ya Juu mkoani Iringa wakionyesha fedha zao baada ya kukabidhiwa na Mgeni Rasmi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa,Mh. Leticia Warioba.
Mgeni Rasmi kwenye hafla ya utoaji wa Tuzo za Excel With Grand Malt kwa vyuo vya Elimu ya Juu mkoani Iringa,Mkuu wa Wilaya ya Iringa,Mh. Leticia Warioba (kushoto) akikabidhi cheti cha Shukrani kwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Tumaini,Prof. Enock Ugulumu kwa kuwezesha wanafunzi wa chuo chake kushiriki shindano hilo.Wapili Kushoto ni Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania,Fimbo Butallah akiwa pamoja na Maofisa wa TBL mkoa wa Iringa.
Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania,Fimbo Butallah akizungumza machache na washiriki wa tuzo hizo kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi.
Mgeni Rasmi kwenye hafla ya utoaji wa Tuzo za Excel With Grand Malt kwa vyuo vya Elimu ya Juu mkoani Iringa,Mkuu wa Wilaya ya Iringa,Mh. Leticia Warioba akizungumza.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Tumaini,Prof. Enock Ugulumu akitoa shukrani zake kwa Mgeni Rasmi na kwa uongozi mzima wa TBL uliofanikisha zoezi hilo.
Mkali wa Muziki wa HipHop nchini,Fareed Kubanda a.k.a Fid Q akiwapagawisha vilivyo mashabiki wake wa mkoani Iringa wakati wa zoezi la utoaji wa Tuzo za Excel With Grand Malt kwa vyuo vya Elimu ya Juu mkoani Iringa.
Wanafunzi wa Vyuo Vikuu mkoani Iringa wakifuatilia zoezi hilo.
Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania,Fimbo Butallah akivuta udongo shimoni wakati wa zoezi la Upandaji Miti katika eneo la Chuo Kikuu Kishiriki cha Mkwawa,Mkoani Iringa jana ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa kauli ya Serikali ya Utunzaji wa Mazingira katika maeneo mbali mbali ya nchini.
Zoezi la upandaji miti likiendelea.
Afisa Mazingira wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Mkwawa,Athuman Said (kulia) akiwaelekeza jambo kwa Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania,Fimbo Butallah (pili shoto) wakati wa zoezi la upandaji miti katika chuo hicho.
No comments:
Post a Comment