HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, June 2, 2012

Spika wa Bunge afungua mafunzo maalum kwa Wenyeviti na Makamu wenyeviti wa Kamati za Bunge

Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akifungua mafunzo maalum yaliyo andaliwa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuwajengea uwezo wenyeviti na makamu wenyeviti wa kamati za Bunge kuchambua Bajeti ya serikali. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya PAC Mhe. John Cheyo na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali Ludovick Uttoh.
Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Ludovick Uttoh akitoa neno la Utangulizi kabla ya kufunguliwa kwa mafunzo maalum ya kuwajengea uwezo wenyeviti na makamu wenyeviti wa kamati za Bunge kuchambua Bajeti ya serikali iliyo andaliwa na Ofisi yake na Kufanyika Bagamoyo leo.
Baadhi ya wenyeviti na makamu wenyeviti wa kamati za Bunge wakifuatilia kwa makini hotuba ya ufunguzi kutoka kwa Mhe. Spika wakati wa mafunzo maalum yaliyo andaliwa kwa ajili yao na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuwajengea uwezo kuchambua Bajeti ya serikali, yaliyofanyika Bagamoyo leo.
Mgeni Rasmi, Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiwa katika picha ya pamoja na wenyeviti na makamu wenyeviti wa kamati za Bunge wanaohudhuria mafunzo maalum yaliyo andaliwa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuwajengea uwezo kuchambua Bajeti ya serikali, yaliyofanyika Bagamoyo leo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad