HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, June 1, 2012

PICHA ZA MATUKIO MBALI MBALI YA RAIS KIKWETE AKIWA JIJINI ARUSHA

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisamiana na Rais wa Japan International Cooperation Agency (JICA) Profesa Akihito Tanaka na baadaye kufanya naye mazungumzo baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Afrika katika ukumbi wa AICC jijini Arusha.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akifanya mazungumzo na Mshauri wa Mfalme wa Tano wa Morocco Bw Omar Kabbaj baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Afrika katika ukumbi wa AICC jijini Arusha.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Makamu wa Rais wa European Investment Bank Bw Plutarchos Sakellaris baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Afrika katika ukumbi wa AICC jijini Arusha Mei 31, 2012.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikagua ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Afrika. Jengo hili liko nyuma ya jumba la mikutano la AICC jijini Arusha.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Afrika. Jengo hili liko nyuma ya jumba la mikutano la AICC jijini Arusha.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na ujumbe wa Zanzibar katika Mkutano Mkuu wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Afrika wakati wa hafla ya chakula cha usiku baada ya ufunguzi wa mkutano huo Mei 31, 2012 usiku katika hoteli ya Ngurdoto Mountain Lodge jijini Arusha
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na vijana wa Arusha walioshiriki kutoa huduma kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Afrika wakati wa hafla ya chakula cha usiku baada ya ufunguzi wa mkutano huo Mei 31, 2012 usiku katika hoteli ya Ngurdoto Mountain Lodge jijini Arusha.PICHA NA IKULU.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad