HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, June 22, 2012

Mkuu wa Wilaya ya Iringa azindua rasmi mradi wa uvunaji maji ya mvua katika Hospitali ya Wilaya ya Iringa


Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Dk. Leticia Warioba akizindua rasmi mradi wa uvunaji maji ya mvua uliopo Hospitali ya Wilaya ya Iringa iliyopo Frelimo mjini humo leo. Mradi huo umefadhiliwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) na kugharimu zaidi ya Shilingi Milioni 50 na unataraji kuwanufaisha wakazi wa eneo hilo zaidi ya 100,000. Wengine kutoka kushoto ni Meya wa Manispaa ya Iringa, Amani Mwamwindi, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa SBL, Teddy Mapunda na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi, Afya na Elimu, V Mushi.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Dk. Leticia Warioba akimshukuru Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), Teddy Mapunda kwa kampuni yake kufadhili mradi huo muhimu wa maji Hospitalini hapo.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Dk. Leticia Warioba akifungua maji kutoka katika tanki moja wapo.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Dk. Leticia Warioba akimtwisha ndoo ya Maji Augusta Mtemi ambaye ni Diwani wa Viti Maalum Iringa ikiwa ni ishara ya uzinduzi huo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad