HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, June 22, 2012

Libeneka la Mtaa kwa Mtaa Lililotembelea Mbagala eneo la Vikunai

Katika pita pita zangu za kuendeleza libeneke la Mtaa kwa Mtaa,niliweza kuibuka katika eneo la Mbagala Vikunai lililopo ubavuni mwa Mbagala Kuu,jijini Dar.haka niliposimama ni kwenye Daraja linalowaunganisha wakazi wa pande mbili za eneo hili la Vikunai,Daraja ambalo limetengenezwa na wakazi wenyewe wa eneo hili kwa kutumia Mabanzi na ni daraja ambalo limetengenezwa kwa kuungwa ungwa na kupachikwa juu ya visiki vya miti iliyokatwa vilivyopo membezoni kwa mto huu.kiukweli kama wewe ni muoga basi huwezi pita katika Daraja hili kwani ukifika katikati linanepa kana kwamba nilavunjia wakati huo.

Madereva wa Boda Boda wakipita juu ya daraja hilo huku wao wakidai kuwa wameshazoea hali hiyo,kwa kawaida kupita hapa ni lazima kusubiriana ila huyu alitaka kujifanya anaharaka sana lakini ilibidi amsubirie mwenzie aende ndio na yeye apite.
Kuna njia nyingine ya Magari,lakini nayo hali yake sio nzuri kwani kutokana na mvua kidogo iliyonyesha hivi karibuni,imesababisha kujaa kwa maji katika sehemu ya njia hiyo,hivyo hakuna gari inayopita tena hapa.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad