KINYWAJI bora cha VitaMalt Plus kinatengezwa na kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kimeonekana dhahiri kuwapagawisha watu wengi katika maeneo mbali mbali nchini,ambao wameweza kukionja.
Kinywaji hicho chenye mchanganyiko wa Ginseng,Aloe Vera na Royal Jelly kwa sasa kinatembezwa mitaani na kuwapa fursa watu mbalimbali kukionja.
Kikiwa hakina kilevi chochote, VitaMalt Plus imeonekana kuwapendeza watu waliofanikiwa kukionja, huku wakifurahi na kudai uwepo wa Vitamin B Complex ni bomba kwao.
Baadhi ya watu waliokuwepo katika baa mbali mbali za jijini Dar ambayo moja yake ni Hongera Bar a.k.a Sebuleni iliyopo Sinza Bamaga, walisema wanashangazwa na ubora wa kinywaji hicho kutokana na uzuri wake.
“Mimi nilipoonja kinywaji hili kusema kweli nimefurahi sana na kwakweli siwezi kukiacha kuanzia sasa,” alisema John Semeye aliyekutwa katika bar maarufu ya Jackie’s iliyopo Masaki, jijini Dar es Salaam.
Alipoulizwa kuhusu hilo, Meneja wa VitaMalt Plus, Consolata Adam alisema wanashukuru kwa kiasi kikubwa kwa kinywaji hicho kupokelewa vema.
“VitaMalt Plus itaendelea kuwa bora zaidi na tunaahidi tutawapa bidhaa bora na yenye kiwango cha kimataifa kila siku.” alisema.



No comments:
Post a Comment