Mambo Basketball team katika kikao kifupi na Public Relations Officer wa ubalozi wa Marekani MS. Dana Banks.
MAMBO BASKETBALL team baada ya kukabidhiwa mipira na Public
Relations Oficcer MS. Dana Banks (mwisho kulia).
MAMBO BASKETBALL imepokea mipira 50 toka Ubalozi wa Marekani leo jijini Dar,Mipira ambayo itatumika katika mafunzo kwa wachezaji wa mpira wa kikapu (Basketball Camps) ambayo yatafanyika katika Miji Ya Mwanza, Musoma,Arusha na Pemba Kati ya Tarehe 18 /6/2012 na tarehe 7/7/2012.
Mambo Basketball kwa niaba ya wadau wote wa mchezo huu hapa nchini tunatoa shukrani zetu za dhani Kwa watu wa Marekani na kuahidi kuendeleza ushiriano uliopo. Mwaka 2009 Waaalimu (Coaches) wa mpira wa kikapu walipewa ziara ya kimafunzo nchini Marekani na kati yao walikuepo watatu toka MAMBO BASKETBALL.
Mambo Basketball ina lengo la kuendesha mafunzo kwa wachezaji mbalimbali nchi nzima haswa wale walioko Mashuleni. Nia kubwa ni kuwawezesha kujiendeleza kimchezo na Kimasomo.
Mwaka Jana mchezaji Alphaeus Kisusi alifanikiwa kupata scholarship na kwa sasa anasoma nchini Canada baada ya kufanya vizuri katika mafunzo yaliendeshwa na Mambo Basketball Ikishirikiana na Tanzania Students Achievement Organisation (TANSAO) pamoja na Newfound Memorial University ya huko Canada.



No comments:
Post a Comment