Mratibu wa Mashindano ya Urembo ya Redd's Miss Kurasini 2012,Yasson Mashaka (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo kwenye ukumbi wa Mgahawa ha Hadd's uliopo Posta jijini Dar es Salaam juu ya shindano hilo litakalofanyika siku ya ijumaa hii ya tarehe 25 / 5 / 2012 katika Ukumbi wa EQUATOR GRILL uliopo mtoni saba saba.Kulia kwake ni Msemaji wa Shindano hilo,Sam Mshana.
Msemaji wa Shindano la Redd's Miss Kurasini,Sam Mshana akiongea na waandishi wa habari.
Baadhi ya warembo watakaoshiriki kwenye Kinyang'anyiro hicho wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Mashindano ya Urembo ya REDD’S MISS TANZANIA 2012 yanaendelea kushika kasi kwa ngazi za vitongoji hasa hapa jijini Dar es salaam, Baada ya kufanyika kwa mashindano katika kituo cha UKONGA, CHUO CHA USTAWI WA JAMII na CHUO CHA FEDHA (IFM) sasa ni zamu ya REDD’S MISS KURASINI 2012.
Redd’s Miss Kurasini 2012 itafanyika ijumaa hii ya tarehe 25 / 5 / 2012 katika Ukumbi wa EQUATOR GRILL uliopo mtoni saba saba.
Jumla ya Warembo kumi na sita mpaka sasa wamejitokeza katika kuwania taji la REDD’S MISS KURASINI 2012 ambalo linashikiliwa na MWAJABU JUMA ambaye pia ni mshindi wa shindano la TOP MODEL 2011 katika fainali za Miss Tanzania 2011, na kwa upamde wa shoo wanafundishwa na ROSE HERBERT ambaye ni mshindi wa Talent katika mashindano ya Miss Tanzania kwa mwaka 2011.
Shindano hili litasindikizwa na bendi ya muziki wa dansi ya FM ACADEMIA (wazee wa ngwasuma) na bibie KHADIJA KOPA mshindi wa tunzo za muziki wa taarabu.
Kiingilio katika shindano hili kimepangwa kuwa shilingi 10,000 kwa kila mtu.
Zawadi kwa washiriki zimepangwa kama ifuatavyo:-
REDD;S MISS KURASINI PESA TASLIM LAKI TANO (500,000.00)
MSHINDI WA PILI LAKI TATU NA NUSU (350,000.00)
MSHINDI WA TATU LAKI MBILI NA NUSU (250,000.00)
MSHINDI WA NNE NA WA TANO KILA MMOJA LAKI MBILI (200,000.00)
WASHIRIKI WOTE WALIOBAKIA KILA MMOJA LAKI MOJA (100,000.00)
Orodha ya majina ya warembo na umri wao ni kama ifuatavyo:-
1. TULEKENE SETH (20) 2. ANGLE GASPER (19)
3. CHRISTINA MOSES (22) 4. ZUHURA SADIKI (21)
5. FLAVIANA MAEDA (22) 6. MWANAISHA ZUBERI (21)
7.FARIDA MROPE (23) 8. IRENE SOSTHENES (20)
9. EDINA MAGIGE (22) 10. SIA KIMAMBO (19)
11. NZELANI JUMA (22) 12. LILIAN JOSEPH (20)
13. ANNA ZAKARIA (21) 14. ASHA MUSA (21)
15. LINDA DEUS 16.BETTY PETER (22)
wadhamini waliojitokeza kufanikisha shindano hili ni pamoja na :-
REDD’S Original, LADY PEPETA, FLEXIP, PJ AMUSEMENT, DODOMA WINE, RENZO SALON, MADIRISHA VIDEO’S PRODUCTION, JAMBO LEO, AUCLAND TOURS AND SAFAARIS, CLOUD’S FM, FATHA KIDEVU BLOG, CAND BUREAU DE CHANGE NA NAEEMS CLASSIC WEAR.




No comments:
Post a Comment