HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, May 23, 2012

Kikao cha Kamati Tendaji ya chama cha Mabunge ya nchi wananchama wa Jumuiya ya Madola kanda ya Afrika (CPA Africa Region) chafanyika jijini Dar es Salaam leo

Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya chama cha Mabunge ya nchi wananchama wa Jumuiya ya Madola kanda ya Afrika (CPA Africa Region) Dk. Patrick Herminie ambaye pia ni Spika wa Bunge la Ushelisheli akiongoza kikao cha siku moja cha kamati hiyo kilichofanyika Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda na Spika wa Bunge la Ghana Mhe. Joyce Bamford – Addo. kushoto ni Naibu Spika wa Cameroon Mhe. Monjowa Lifaka, katibu wa Bunge la Ghana Emmanuel Anyimadu na Mkurugenzi wa Habari, Elimu kwa Umma na Uhusiano wa Kimatifa wa Bunge Jossey Mwakasyuka.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiwa katika mazungumzo na katibu wa Bunge la Ghana Emmanuel Anyimadu (kulia) kabla ya kuanza kwa mkutano wa Kamati tendaji ya (chama cha Mabunge ya nchi wananchama wa Jumuiya ya Madola kanda ya Afrika (CPA Africa Region) uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkurugenzi wa Habari, Elimu kwa Umma na Uhusiano wa Kimatifa wa Bunge Jossey Mwakasyuka.Picha na Owen Mwandumbya wa Bunge.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad