Mshindi wa tuzo ya Wimbo Bora wa Zouk Rhumba,Ali Kibaa akikabidhiwa tuzo yake na Mwanadada Dina Marios wa Clouds Fm na Mkongwe Rainfred Masako wa ITV.
Muwakilishi wa kundi la Arusha Gold akipokea tuzo ya Wimbo bora wa Ragga,kutoka kwa mwanadada Khadija Mwanamboka.
Wasanii wa Muziki wa Ragga kutoka jijini Arusha wafahamikao kwa jina la Arusha Gold wakitoa shukrani kwa wadau wao waliowapigia kura mpaka kupata ushindi huo.
Mshindi wa tuzo ya Dancehall,Quen Darlin akiifurahia tuzo yake mara baada ya kukabidhiwa usiku huu.
Waendeshaji wa hafla hii usiku huu ni Milard Ayoo na mwanadada Vanessa Mdee.
Burudani kutoka kwa vijawa T.H.T.
Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar usiku huu ukiwa umefurika kwa washabiki wa muziki nchini ikiwa ni siku ya utoaji wa tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2012.
Mchekeshaji wa Ze Komedi,Mpoki akitambulisha moja kikundi ya utumbuizaji usiku huu.
No comments:
Post a Comment