Mtanzania aishie nchini Trinidad and Tobago akifanya shughuli zake za ujasilia mali Bi. Grace Mongi – Clifton akimkaribisha Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda mara alipomtembelea Nyumbani kwake nchini Trinidad and Tobago. Mhe. Spika alikuwa nchini humo kuhudhuria Mkutano wa 21 wa Maspika wa nchi za Jumuiya ya Madola uliofanyika nchini Trinidad and Tobago
Bi. Grace Mongi – Clifton akimkabidhi Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda kitabu alichokiandika kiitwacho Face to Face with the Prince of Darkness ikiwa ni mojawapo ya kazi zake. Bi Mongi anatarajia kuja kuzindua kitabu chake mwezi machi 2012 hapa nchini. Mhe. Spika alikuwa nchini humo kuhudhuria Mkutano wa 21 wa Maspika wa nchi za Jumuiya ya Madola uliofanyika nchini Trinidad and Tobago
Bi. Grace Mongi – Clifton akifurahia khanga aliyopewa na Mhe. Spika mara baada ya Mhe. Spika kumtembelea Mtanzania huyo nchini Trinidad and Tobago. Mhe. Spika alikuwa nchini humo kuhudhuria Mkutano wa 21 wa Maspika wa nchi za Jumuiya ya Madola uliofanyika nchini Trinidad and Tobago.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiwa na Maspika wenzie kutembelea vivutio mbalimbali vya kitalii katika Mji wa Port of Spain katika visiwa vya Trinidad and Tobago mara baada ya kumalizika kwa kumtano wa 21 wa Maspika wa nchi za Jumuiya ya Madola uliofanyika nchini humo.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiwa na Maspika wenzie kutoka nchi wananchama wa Jumuiya ya Madola wakifuatilia maelezo ya shughuli za uchimbaji mafuta na gesi asilia kutoka kwa mwenyekiti wa kampuni ya kuchimba mafuta ya nchi hiyo (hayupo pichani) mara baada ya kuitembelea kampuni hiyo kujionea shughuli zake.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akifurahia sanamu katika msikiti mkubwa wa madhehebu ya dini ya KIHINDU uliopo Port of Spain Nchini Trinidad and Tobago wakati wakitembelea vivutio mbalimbali vya utalii nchini humo baada ya kumalizika kwa kumtano wa 21 wa Maspika wa nchi za Jumuiya ya Madola uliofanyika nchini humo.
No comments:
Post a Comment