HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, January 12, 2012

SAFARI LAGER YATANGAZA KUDHAMINI MASHINDANO YA TAIFA YA VISHALE (DARTS)

Meneja wa bia ya Safari Lager,Oscer Shelukindo akikabidhi ubao wa mchezo wa vishale (Darts Boad) kwa Mwenyekiti wa Mchezo wa Vishale (Darts) Taifa, Gesase Waigama ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa Mashindao hayo ya Taifa yanayotaraji kuanza kesho Mkoani Dodoma.Kushoto ni Mratibu wa Mashindano hayo,Innocent Melleck
Meneja wa bia ya Safari Lager,Oscer Shelukindo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa kutangaza udhamini wa mashindano ya Taifa ya mchezo wa vishale (Darts) yanayotaraji kuanza kesho mkoani Dodoma.Kulia ni Mwenyekiti wa Mchezo wa Vishale (Darts) Taifa, Gesase Waigama.
Mwenyekiti wa Mchezo wa Vishale (Darts) Taifa, Gesase Waigama akizungumzia maandalizi ya mashindano ya Taifa ya mchezo huo,yanayotaraji kuanza kutimua vumbo hapo kesho mkoni Dodoma.Kulia ni Meneja wa bia ya Safari Lager,Oscer Shelukindo

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager imetangaza rasmi kudhamini mashindano ya Taifa ya Darts yanayotarajiwa kuanza kesho tarehe 13.01.2012 mpaka .15.2012 mkoani Dodoma.

Akitangaza udhamini wa jumla ya Mil. 30 kwa mashindano hayo, Meneja wa bia ya Safari Lager, Ndugu Oscar Shelukindo alisema “Bia ya Safari lager imekamilisha yale mahitaji yote muhimu ya Timu ikiwa ni pamoja na zawadi mbalimbali zitakazotolewa kwenye mashindano hayo yatakayofanyika kwa muda wa siku tatu mkoani Dodoma kwenye ukumbi wa Rose Garden uliopo eneo la Area C.

Alisema lengo kuu la bia ya Safari kudhamini mashindano hayo ni katika kufanikisha kuwa mchezo wa Darts unakuwa miongoni mwa michezo mikubwa nchini na kupata timu bora ya Taifa itakayofanikisha kuliletea Taifa heshima kwenye michezo ya kimataifa.

Alisema mchezo wa Darts ni mchezo mzuri ambao unahitaji kuungwa mkono na wadau wote wapenda michezo ili kuweza kufikia malengo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwa na vilabu vyenye nguvu na hayo yanawezekana kama kutakuwa na ushirikiano baina ya wadau wa michezo katika kuunganga mkono juhudi za kukuza na kuendeleza mchezo huo nchini

Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha Darts nchini Bwana Gesase Waigama aliishukuru Tbl kupitia bia ya safari kwa juhudu na msaada mkubwa wanaoutoa katika kuhakikisha mchezo huo unapata mafanikio nchini na kupelekea Tbl kuwa mfano wa kuigwa katika kuendeleza michezo nchini.”Tunaishukuru sana Tbl Kupitia bia yake bora ya Safari kwa juhudi na msaada mkubwa wanaoutoa kwetu katika kuhakikisha mchezo wa Darts unakuwa na kuheshimika nchini ,huu ni mchango unaopaswa kuheshimika na kuthaminiwa na watu wote wenye nia nzuri na michezo nchini”

Alisema kwa mwaka huu michezo itachezwa kwa mtindo wa ligi na kutakuwa michezo ya aina mbili ikiwa ni Timu za mikoa na michezo ya mchezaji mmojammoja na wale watakaoibuka washindi watapata zawadi mbalimbali ikiwa ni pamoja na fedha taslimu na vikombe.

Alisema mikoa itakayoshiriki mashindano hayo kwa mwaka huu ni pamoja na mikoa ya Ilala,Temeke,Kinondoni,Tanga,Morogoro,Arusha,Kilimanjaro,Mbeya,Mwanza na Dodoma ambapo jumla ya timu 30 zimeshawasili mkoani Dodoma tayari kwa kuanza mashindano hayo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad