HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, January 18, 2012

RAIS KIKWETE AONGOZA MAMIA KATIKA MAZISHI YA REGIA MTEMA MJINI IFAKARA LEO

 Rais Jakaya Kikwete akiweka shada la maua kwenye kaburi la Marehemu Regia Mtema ambaye alikuwa Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA) Jimbo la Morogoro aliefariki kwa ajali ya gari maeneo ya Ruvu mkoani Pwani hivi karibuni .Rais Kikwete ameongoza mamia ya Waombolezaji wa mji wa Ifakara kwenye mazishi hayo leo ambapo pia viongozi mbali mbali walishiriki.
Rais Jakaya Kikwete akiweka udongo kwenye kaburi la Marehemu Regia Mtema aliezikwa leo Ifakara Mkoani Morogoro.
Rais Jakaya Kikwete akiwa kwenye mazishi ya Marehemu Regia Mtema yaliyofanyika Ifakara leo.Wengine pichani ni Spika wa Bunge,Mh. Anne Makinda (pili kulia),Naibu Spika wa Bunge,Mh. Job Ndugai (kulia),Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,Mh. Joel Bendera (pili kushoto) pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni,Mh. Freeman Mbowe.Picha na Ikulu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad