Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza na wakandarasi wa Kampuni ya Aasleff Bam International ya Uholanzi inayojenga barabara ya Laela - Sumbawanga kwa kiwango cha lami katika Mkoa huo. Mkuu huyo wa Mkoa alilazimika kufanya ziara kujionea hali ya ujenzi inavyoendelea pamoja na kuzungumza na wafanyakazi wa Kampuni hiyo. Kulia ni Mashine aina ya mixer inayochanganya udongo na cement na kunyoosha barabara kabla ya kokoto ngumu na lami kuwekwa. Injinia Manyanya akishikana mikono na mmoja wa makandarasi wa Aasleff Bam mara baada ya kupewa maelezo juu ya mashine inayoonekana nyuma yao ya kuchanganya udongo na cement. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Kanali John Antonyo Mzurikwao na Kushoto ni Meneja wa Tanroads Mkoa wa Rukwa Kabaka Florian Mwombeki.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wazawa wa kampuni ya Aasleff Bam International ya Uholanzi inayojenga barabara ya Laela - Sumbawanga kwa kiwango cha lami. Aliomba kuzungumza na wafanyakazi hao kutokana na kulaumiwa kuiibia kampuni hiyo vifaa ikiwepo mafuta ya diesel zaidi ya lita 30,000, tani 40 za simenti , na nondo zaidi ya tani 300.
Mkuu huyo wa Mkoa aliwaasa wafanyakazi hao kuwa na moyo wa kizalendo kwa kuona kuwa kazi anayofanya kandarasi huyo italeta manufaa kwao. Alitangaza vita na yeyote yule atakayethibitika kuhusika na wizi katika kampuni hiyo pamoja na kampuni zingine zinazofanya kazi hiyo ya ujenzi Mkoani Rukwa. Alisema kuwa ni aibu kuona wizi wa namna hiyo kwani kazi anayofanya kandarasi huyo ni kwa manufaa ya watanzania wenyewe.
No comments:
Post a Comment