HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, January 16, 2012

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL MGENI RASMI SHEREHE ZA KUUKARIBISHA MWAKA MPYA WA KICHINA JIJINI DAR ES SALAAM

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati wa sherehe za kuukaribisha mwaka mpya wa Kichina, zilizoandaliwa na Chama cha Wafanyabiashara wa Kichina nchini (CBCT), zilizofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam jana jioni.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea mfano wa Hundi, yenye thamani ya Sh. Milioni 16, kutoka kwa Balozi wa China nchini Tanzania, Liu Xinsheng, (kulia) iliyotolewa na City Bank Tanzania LTD kwa ajili ya kusaidia waathirika wa mafuriko yaliyotokea jijini Dar es Salaam mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka jana, ikiwa ni sehemu ya sherehe za kuukaribisha mwaka mpya wa Kichina zilizofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam jana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea mfano wa Hundi, yenye thamani ya Sh. Milioni 10, kutoka kwa Balozi wa China nchini Tanzania, Liu Xinsheng, (kulia) iliyotolewa na Chama cha Wafanyabiashara wa Kichina wa Tanzania (CBCT) kwa ajili ya kusaidia waathirika wa mafuriko yaliyotokea jijini Dar es Salaam mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka jana, ikiwa ni sehemu ya sherehe za kuukaribisha mwaka mpya wa Kichina zilizofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam jana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya wasanii wa Kichina waliokuwa wakitoa burudani jukwaani wakati wa sherehe hizo, wakati akijiandaa kuondoka katika Viwanja hivyo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza jambo na Balozi wa China nchini Tanzania, Liu Xinsheng , wakati alipohudhuria sherehe za kuukaribisha mwaka mpya wa Kichina, zilizoandaliwa na Chama cha Wafanyabiashara wa Kichina nchini (CBCT), zilizofanyika jana jioni, kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Makamu Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongoza na Balozi wa China nchini Tanzania, Liu Xinsheng, wakati akiwasili kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jinni Dar es Salaam jana jioni, katika sherehe za kuukaribisha mwaka mpya wa Kichina, sherehe zilizoandaliwa na Chama cha Wafanyabiashara wa Kichina nchini (CBCT). Picha na Muhidin Sufiani-OMR.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad