HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, January 11, 2012

MADHARA YA BOMBA LA MAFUTA LA TANZANIA NA ZAMBIA (TAZAMA) WILAYANI KILOSA,MH. MALIMA AITAKA TAZAMA KUWAJIBIKA

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam Malima ( wapili kutoka kulia waliochuchumaa ) akipata maelezo ya madhara ya mafuta yaliyoingia kwenye chanzo cha maji katika Skimu ya Umwagiliaji ya Malolo kutoka kwa wataalamu wa Tazama na Watendaji wa Serikali ya Wilaya ya Kilosa, Mkoa wa Morogoro kuangalia  madhara yaliyosababishwa na mafuta yaliyomwagikia ndani ya chanzo cha mto na skimu ya umwagiliaji Kata ya Malolo.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam Malima  akiwa na wataalamu wa Tazama na Watendaji wa Serikali ya Wilaya ya Kilosa,Mkoa wa Morogoro kugalialia madhara yaliyosababishwa na mafuta yaliyomwagikia ndani ya chanzo cha mto na skimu ya umwagiliaji Kata ya Malolo.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam Malima (katikati) akifafanua jambo kwa wataalamu wa Tazama na Watendaji wa Serikali ya Wilaya ya Kilosa, Mkoa wa Morogoro baada ya kukagua madhara yaliyosababishwa na mafuta yaliyomwagikia ndani ya chanzo cha mto na skimu ya umwagiliaji Kata ya Malolo.

Katika sakata hilo , Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam Malima,ametoa siku tatu kuanzia Januari 13, mwaka huu kwa Uongozi wa Tazama kupeleka timu ya wataalamu kutoka Tume ya Mamlaka ya Mazingira, Afya na wachunguzi wa udongo kuweza kuchukua sampuli kwa ajili ya kuzifanyia uchunguzi wa kina ili kuweza kubaini madhara yatokanayo na mafuta hayo.

Kwa wananchi wenye kulalamika wanawashwa mwili na macho , vipimo vichukuliwe kwa ajili ya uchunguzi wa kimaabara kuanzisha chanzo cha muda cha maji ya mseleleko kwa ajili ya matumizi ya wananchi wa Kata
hiyo wakati wakisubiri kupata taarifa ya usalama wa maji yaliyochafuliwa na mafuta.

Hata hivyo ameutaka Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa , nao kuchukua sampuli hizo ili kuchunguza na majibu yatakayotolewa yawezekuoanishwa na yatakayoletwa na Wataalamu wataowezeshwa na Tazama ili pasiwe na hofu ya kupikwa kwa matokeo ya uchunguzi huo

Pia ameutaka uongozi wa Tazama kuandaa mpango mkakati wa utekelezaji utakaowezesha kuwafidia wananchi wa Kata hiyo kutokana na madhara na kuuwasdilisha Ofisini kwake Januari 12, mwaka huu na pia majibu ya uchunguzi yatolewe mbele ya wananchi wa Kata hiyo kwa kuwashirikisha viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa.Picha na Habari na John Nditi wa Globu ya Jamii,Morogoro.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad