Wanafunzi Wa Udom Wakionyesha Furaha Kwa njia tofauti tofauti wakati wa kuukaribisha mwaka mpya 2012 usiku wa kuamkia leo
Kijana huyu alijitoa Mhanga na kutoa sub woofer yake na laptop na kuweka disco vumbi na vijana kuanza kujiachia kila mtu kwa staili yake zote hizo zikiwa ni shamrashamra za kuupokea mwaka mpya 2012.
Hapa vijana wakiserebuka kila mtu kwa staili yake wengi ni kama wanavyoonekana katika picha
Hawa ni wanafunzi wa chuo kikuu cha dodoma wakiserebuka rumba wakati wa shamrashamra za kuukaribisha mwaka mpya 2012 usiku wa kuamkia leo
Hapa wadau wengine walikua wakimzonga dj wakitaka awawekee viduku ili wajimwage.
Huku wengine wakisakata boringo huku wengi wapo kwenye mduara yaani kila mtu na staili yake yote tu ni furaha za kuupokea mwaka kwa shangwe za aina yake
Huku wengine wakicheza mchezo wa utotoni wa Ukuti Ukuti yote ni furaha tu na shangwe za kuupokea mwaka mpya 2012 usiku wa kuamkia leo.
Huku wengine wakicheza kwaito yote ni shamrashamra za kuupokea mwaka mpya 2012
Michezo mingine ni ya hatari kweli.Kijana huyu ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja akijitoa ufahamu na kuzuia gari kwa kichwa lisipite mahala ambapo wanafunzi walikusanyika kusheherekea kuupokea mwaka mpya 2012 usiku wa kuamkia leo
Huku wengine wakidandia magari yaliyokuwa yakikatiza sehemu ambapo wanafunzi walikusanyika kusherehekea kuupokea mwaka mpya 2012
Wadau wa UDom wakiwa wamejiachia Bila shida katika shamra shamra za kuukaribisha mwaka mpya ndani ya UDOM
Kutoka Disco vumbi hadi ndani ya Cafteria ya Break Point wadau wakiserebuka kwa nguvu zote katika shamra shamra za kuupokea mwaka mpya 2012 ndani ya UDOM
Huku wengine wakijilaza barabarani kuzuia magari yasikatize eneo ambalo wanafunzi walikusanyika kusherehekea kuupokea mwaka
Hapa napo disco vumbi likiendelea na kila mmoja na staili yake hakuna kumuiga mwingine.Picha zote na Lukaza Blog.
No comments:
Post a Comment