HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, January 19, 2012

breaking nyuzzzzz: Mh. Jeremia Sumari afariki dunia leo

TAARIFA ya iliyotufikia hivi punde katika inaeleza kuwa mbunge wa jimbo la ARUMERU kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM),Mh. Jeremia Sumari (pichani) amefariki Dunia asubuhi hii mara baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Mh. Jeremia Sumari ni mbunge wa pili kufariki dunia kwa mwaka huu 2012 kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kutanguliwa na Mbunge wa Viti Maalum kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoa wa Morogoro,Marehemu Regia Mtema aliyezikwa nyumbani kwao Ifakara Mkoani Morogoro jana na mazishi yake yaliongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh. Dkt. Jakaya Kikwete.

Tunaendelea kufuatilia taratibu zote za msiba huu na tutaendelea kutoa taarifa kadri zitakavyokuwa zikitufikia.

Mungu ailaze roho za marehemu mahala pema peponi 

-Amein

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad