HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, January 9, 2012

BancABC YATOA MSAADA WA VIFAA VYA SHULE KWA WAATHIRIKA WA MAFURIKO DAR ES SALAAM

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick, akipokea baadhi ya vifaa vya shule kwa ajili ya waathirika wa mafuriko kutoka kwa Bi. Ruth Makombe, Mkuu wa Kitengo cha Biashara za Rejareja  na Ujasiriamali, wa BancABC.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick, katika picha ya pamoja na wanyakazi wa BancABC baada ya kupokea msaada.
Baadhi ya vifaa vya shule vilivyotolewa na BancABC kwa wanafunzi ambao familia zao zilikumbwa na maafa.

BancABC imetoa msaada wa sare za shule, viatu, madaftari na vifaa vingine mbalimbali ili kuwasaidia waathirika wa mafuriko walioko katika kambi mbalimbali jijini Dar es salaam.
Akikabidhi msaada huo, Bi. Ruth Makombe ambaye ni Mkuu wa kitengo cha Biashara za Rejareja na Ujasiriamali (Head of Retail & SME Banking) wa benki hiyo amesema kuwa BancABC inatambua mahitaji ya waathirika hao kuwa ni mengi lakini wametoa kipaumbele kwa  elimu katika wakati huu kwani ndio nguzo pekee ya kuwakomboa watoto pamoja na wazazi wao kwa maisha ya baadaye.
Awali,  Afisa Masoko wa Benki hiyo, Bi. Evelyn Auguste  amesema kuwa benki hiyo imeona ni vyema kuitikia wito wa waathirika wa mafuriko kwa kutoa msaada huo wa vifaa vya shule katika wakati huu ambapo shule zinafunguliwa ili kukidhi mahitaji ya wanafunzi ambao wazazi wao hawana uwezo wa kuwanunulia vifaa hivyo kwa sasa.
Akipokea msaada huo, Mkuu wa Mko wa Dar es Salaam, Bw. Said Meck Sadick amesema kuwa msaada  huo umekuja katika muda muafaka kwani wanafunzi na wazazi wako katika maandalizi ya kuanza mwaka mwingine wa masomo na kutoa wito kwa wadau wengine kutoa misaada ya mahitaji ya shule.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad