HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, December 23, 2011

Ziara ya Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara wa Nishati na Madini kwenye maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko jijini Dar es Salaam

Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Bw. Eliakim C. Maswi akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa wakazi wa eneo la Mbagala Kingugi mara baada ya kutembelea eneo hilo kwa ajili ya kujionea uharibifu wa miundombinu ya umeme uliosababishwa na mafuriko yaliyotokea tangu juzi. Aidha aliambatana na Mkurugenzi wa Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) Eng. William Mhando pamoja na wataalamu kutoka katika shirika hilo na makao makuu ya Wizara ya Nishati na Madini.
Msikiti wa Mbagala Kingugi ni moja ya nyumba tano zilizoharibiwa kabisa na mafuriko hayo. Aidha nyumba nyingine 15 zimebomolewa kiasi.
Mkurugenzi wa Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) Eng. William Mhando alilazimika kuingia kwenye lori la TANESCO na kujaribu kulitoa lori hilo lililokuwa limekwama kwenye maeneo ya Mbagala Kingugi. Lori hilo lililokuwa limebeba nguzo limekwama tangu jana. Nguzo hizo zilikuwa ni kwa ajili ya kukarabati miundombinu ya umeme iliyoharibika.
Mmoja wa wakazi walioharibikiwa na nyumba zao akimpatia maelezo Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Bw. Eliakim C. Maswi jinsi nyumba yake ilivyoharibiwa.
Gari la Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) likijaribu kuvuta gari lenzake lililokwama kwenye tope wakati likipeleka nguzo za umeme kwenye eneo la Mbagala Kingungi kwa ajili ya kukarabati miundombinu iliyoharibiwa na mafuriko.
Mkazi wa eneo la Jangwani jijini Dar es Salaam aliyejulikana kwa jina la Tyson akimpatia maelezo Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Bw. Eliakim C. Maswi juu ya uharibifu wa mali zao ikiwamo nyumba uliosababishwa na mafuriko.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad