Wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Kishiriki, Muhimbili (MUHAS) wakimsikiliza mwenzao kabla ya kusambalatishwa na kikosi kazi cha Jeshi la Polisi (FFU).
Na Francis Dande
Wanafunzi
wa Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Kishiriki, Muhimbili (MUHAS), leo
wamesababisha shughuli za Mahafali ya Tano ya Chuo hicho kusimama kwa
muda baada ya kuzuka kwa fujo kubwa zilizopelekea Askari wa Jeshi la
Polisi kutumia mabomu ya kishindo ili kuwatawanya.
Wanafunzi
hao walikuwa wakiimba nyimbo mbalimbali za kuhamasishana huku wakiwa na
mabango yenye ujumbe mbalimbali kwa lengo la kuushinikiza uongozi wa
chuo hicho kurudisha serikali ya wanafunzi (MUHASSO).
Mwenyekiti
wa Baraza la Chuo hicho, Deogratias Ntukumazina alitoa ahadi kwa
wanafunzi hao ya kuirudisha Serikali ya Wanafunzi pindi watakapofuta
kesi waliyofungua Mahakama Kuu kauli ambayo ilipingwa vikali na
wanafunzi hao na kutishia kuvuruga shughuli za mahafali zilizokuwa
zimesimama kwa muda kutokana na wanafunzi hao kufanya mkutano wao
uongozi wa Chuo mbele ya Jukwaa ambalo sherehe za kuwatunuku wahitimu
zingefanyika kutokana na kugoma kuondoka mahali hapo hata baada ya
uongozi wa Chuo kuwataka kufanya hivyo jambo ambalo lilisababisha Jeshi
la Polisi kuongeza nguvu ili kuwatawanya.
Hali
ilivyokuwa mbaya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile
alitoa amri kwa Polisi waliokuwa wakilinda Usalama kutumia nguvu jambo
ambalo lilisababisha baadhi ya wazazi waliofika katika mahafali hayo
kukimbia ovyo na kuanguka na watoto na kusababisha baadhi yao kuumia
kutokana na mawe yaliyokuwa yakirushwa na wanafunzi na baadhi ya viti
kuvunjwa na wanafunzi hao, katika kurupushani hiyo baadhi ya wanafunzi
walikamatwa na Polisi.
Katika
Mahafali hayo ambayo baadaye yalifanyika chini ya ulinzi mkali baada ya
polisi kuwatawanya wanafunzi hao baada ya njia ya majadiliano
kushindikana kutokana na jazba za wanafunzi hao waliokuwa walikuwa
wakidai serikali ya wanafunzi ilirudishwe leo.
Hata
hivyo Kwa mujibu wa mmoja wa wanafunzi hao aliyetambulika kwa jina la
Njechele Boniface alisema kuwa walianza kukusanyika chuoni hapo majira
ya saa mbili asubuhi ili kufanya mkutano wao na Mwenyekiti wa Baraza la
Chuo, Deogratias Ntukumazina ili kuepuka kuingiliana na shughuli za
mahafali hayo lakini Mwenyekiti wa Baraza la Chuo alifika chuoni hapo
majira ya saa sita mchana na kusababisha kuingiliana kwa mkutano huo na
shughuli za mahafali hayo.
mabango.
malalamiko.
Brass Band ya Jeshi la Magereza ikitumbuiza kabla ya kuzuka kwa vurugu hizo.
Wakuu
wa Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Kishiriki, Muhimbili
(MUHAS) wakiingia kwa maandamano kwenye Mahafali ya Tano ya Chuo hicho
kabla ya kuzuka kwa vurugu.
Baadhi ya Wahitimu wa Chuo hicho wakiwa tayari kwa kutunukiwa nishani zao kabla ya kuzuka kwa vurugu.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS),Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Mh. Ali Hassan Mwinyi (katikati) akiongozana na baadhi ya wakuu wa Chuo hicho mara baada ya kuzuka kwa vurugu za wanafunzi wa chuo hicho waliokiwa wakitaka kurudishwa kwa Serikali ya Wanafunzi ambayo ilivunjwa hapo awali.
Mmoja wa wanafunzi wa Chuo hicho akiwa ametiwa mbaroni na Askari Polisi.
Mmoja wa watu walioathirika na vurugu zilizotokea leo akiwa ameanguka katika kiti.
Askari Polisi akiwa na tayari lolote.
Askari Polisi wamekasirika sasa ni mwendo wa macho mbele.
Askari Polisi akiwa tayari kwa lolote.
Kamanda wa polisi mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile akiwasihi wanafunzi kutawanyika.
wazee wakiwa tayari kwa lolote
i hope the message have been delieved
ReplyDelete