wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Eckernforde Tanga Univesity kilichopo Jijini Tanga, wakimzonga Mshauri wa wanafunzi wa chuo hicho 'Dean Of Students' Bw Zawadiel Mkilindi kufuatia mzozo mkubwa ulioibuka chuoni hapo kuhusu kusimamishwa masomo wanafunzi 11 ambao walikosa mkopo kutoka bodi ya mikopo hivyo uongozi wa chuo kuwapa barua ya kuwataka kuondoka chuoni hapo.
Makamo
wa rais wa serikali ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Eckernforde Tanga
Univesity Bw Santus Tangatya akiwasomoea wanafunzi wenzake barua ambayo
wanafunzi 11 waliokosa mikopo ya bodi ya mikopo wakitakiwa kundoka
chuoni hapo licha ya wanafunzi wenzao kuwachangia sehemu ya mikopo hiyo
ili waendelee kubaki lakini uongozi wa chuo uling'ang'ania kutaka
kuondoka.
"Tumechanga
shilingi 100,000 kila mtu ili wezetu waziondoke chuoni lakini uongozi
wamegoma na wameona barua hii eti wenzetu 11 waondoke, sisi kama
viongozi wenu mliotuchagua tunasema hatukubali na hatutaingia darasani
hadi hatma ya wenzetu hawa ambao wamewalazimisha warudie mwaka kwasababu
ya kukosa mikopo, hawakubali wametumia ubabe tu," Makamo wa rais wa
serikali ya chuo kikuu cha Eckernforde tanga univesity Bw. Santus
Tangatya akiwaeleza wanafunzi wenzake waliokusanyika kwenye bustani za
chuo hicho.
Mshauri
wa wanafunzi "Dean Of Students' Bw. Zawadiel mkilindi wa kwanza kushoto
akitoa maelezo ni kwanini uongozi wa chuo cha Eckernforde Tanga
Univesity umewapa barua za kuwataka kurudia mwaka wanafunzi 11 kati ya
64 wa mwaka wa pili wanaochukua shahada ya elimu kufuatia kukosa mikopo
kutoka bodi ya mikopo nchini, lakini hata hivyo wanafunzi hao
hawakukubaliana na maelezo yake.Picha na Mashaka Mhando,Tanga
No comments:
Post a Comment