HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, December 30, 2011

Wakulima wa zao la Karafuu Kisiwani Pemba watakiwa kutokuwa na wasi wasi wakuteremka kwa bei ya zao hilo

Na Marzouk Khamis - Maelezo Pemba.

Wakulima wa zao la Karafuu Kisiwani Pemba wametakiwa kutokuwa na wasi wasi wakuteremka kwa bei ya zao hilo na badala yake Shirika la Taifa la Biashara Zanzibar(ZSTC) litaendelea kununuwa zao hilo kwa bei iliopo hivi sasa.

Kauli hiyo imetolewa na Afisa Mdhamini Wizara ya Biashara , Viwanda na Masoko Pemba Hemed Suleiman Abdulla alipokuwa akizungumza LEO na Waandishi wa Habari wa vyombo mbali mbali Kisiwani Pemba huko katika Ukumbi wa Kiwanda cha Makonyo Chake.

Amesema kuwa uvumi uliozagaa kuwa Karafuu zitateremshwa bei sio kweli na kwamba Serikali inawahakikishia wakulima kuwa bei ya zao hilo ipo pale pale kama ilivyotangazwa hapo kabla na
Wananchi wametakiwa kutokuwa na wasiwasi wowote ule .

Afisa Mdhamini huyo amewataka Wananchi kuithamini kauli iliotolewa na Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein kuwa kamwe Karafuu hizotoshushwa bei hata kama zitateremka bei katika soko la Dunia basi Serikali ya Mapinduzi Zanzibar itaendelea kununua kwa bei hiyo hiyo kwa kuwapatia Wakulima asilimia 80 ya bei itakayonunuliwa.

Kwa hivyo amewataka Wakulima kutobabaishwa na watu wachache ambao hawaitakii mema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwani wao malengo yao ni kutaka kusafirisha zao hilo kwanjia ya Magendo.

Akizungumzia juu ya Ununuzi wa zao la Karafuu Hemed amesema kuwa ZSTC itaanza tena kununuwa Karafuu katika vituo vyake vyote kuanzia jumaatatu ijao kama kawaida na kusema kuwa kabla yakusiotishwa ununuzi wa Karafuu hizo hapo tarehe 24 mwezi huu jumla ya Tani 3391 zenye thamami ya shs Billioni hamsini,laki sita na arobaini na mbili millioni mia saba kuminatano elfu zimeshanunuliwa.

Amesema kuwa mpaka sasa Shirika tayari limeshavuka lengo lililojiwekea ya Ununuzi wa Karafuu katika msimu huu ambapo ilikisia kununuwa tani 2770. .

Kutona la ununuzi huo Afisa Mdhamini huyo amesema kuwa hivi sasa Wakulima wa Pemba wa zao la Karafuu wameshajipatia jumla ya shs billioni 50 Mia Sita aroubaini na mbili Millioni laki saba na kuminatano elfu ambazo zimo mikononi mwao.

Aidha Hemed amewapongeza Wakulima ,Wanananchi pamoja na Waandishi wa Habari Kisiwani Pemba kwa kazi nzuri walioifanya katika kipindi chote cha Ununuzi wa zao hilo na akawataka kuendelea kushilrikiana na ZSTC kwani karafuu zinaonekana bado zingalipo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad