Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya Vodacom Tanzania Bw. Salum Mwalim na Afisa wa Mfuko wa Kusaidia Jamii wa kampuni hiyo Bi. Grace Lyon wakishusha viloba vya mchele, unga wa sembe,sukari na maharage vilivyotolewa na Vodacom kusaidia kambi ya waathirika wa mafuriko ya Dar es salaam ya Hananasifu juzi. Wa kwanza kulia ni Mfanyakazi wa Vodacom Lilian Kisamba akisadiana na wasimamizi wa kambi hiyo kupokea vyakula hivyo.
Mkuu
wa Vodacom Foundation Bw. Yessaya Mwakifulefule akimtiwsha Mjumbe wa
Serikali ya Mtaa wa Mkunguni B, kata ya Hananasifu Bw. Andrew Mkude
kiloba cha sukari. Vodacom ilikabidhi mchele, sukari, unga wa sembe,
mikate na maji ya kunywa kwa waathirika wa maafa ya Dar es salaam
wanaojihifadhi katika kambi ya Hananasifu juzi.
Afisa
wa Vodacom Foundation Grace Lyon akisaidiana na mmoja wa wasimamizi wa
kambi ya waathirika wa maafa ya Dar es salaam kambi ya Green Acre
Magomeni kubeba kiloba cha mchele tayari kukabidhiwa kwa waathirika.
Vodacom ilitoa msaada wa vyakula kambini hapo ikiwemo mchele, sukari,
unga wa sembe, mikate na maji ya kunywa juzi.
Mfanyakazi
wa Vodacom Bi. Lilian Kisamba akisaidiana na mmoja wa wasimamizi wa
kambi ya waathirika wa maafa ya Dar es salaam kambi ya Green Acre
Magomeni kubeba kiloba cha mchele tayari kukabidhiwa kwa waathirika.
Vodacom ilitoa msaada wa vyakula kambini hapo ikiwemo mchele, sukari,
unga wa sembe, mikate na maji ya kunywa juzi.
No comments:
Post a Comment