Msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya,Sir Juma Nature pichani kati akishiriki uzinduzi wa Airtel Money ndani ya mji wa Dodoma jioni ya jana kwenye uwanja wa Jamhuri,ambapo watu mbalimbali walijitokeza kwa wingi kulishuhudia tukio hilo adhimu,kulia ni Meneja Mawasiliano wa kampuni ya Airtel, Jackson Mmbando na kushoto ni Meneja wa Airtel Money-Tanzania,Asupya Bussi Nalingingwa.
Mmoja wa wasanii wa miondoko laini laini hivi,aitwaye Mr Blue a.k.a Kabaisa akitumbuiza jukwaani jioni ya jana kwa wakazi wa mji wa Dodoma waliojitokeza kwa wingi kwenye tamasha la uzinduzi wa Airtel Money.
Mmoja wa sanii mahiri wa miondoko ya hip hop hapa bongo,Hamis Mwinyjuma a.k.a Mwana FA akiwapagawisha baadhi ya wakazi wa mji wa Dodoma waliofika jioni ya jana kwenye tamasha la uzinduzi wa huduma ya Airtel Money,uliofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri,mjini Dodoma na kuhudhuriwa na wati kibao.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Q-Chilla a.k.a Savimbi akiwaimbisha washabiki wake jioni ya jana kwenye uwanja wa Jamhuri wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel Money.
Anajiita Simba Dume ndani ya msitu mnene,ni mmoja ya Wasanii wakongwe wa hip hop hapa nchini,ndani ya miondoko ya muziki wa kizazi kipya,Mfalme wa rhymes Afande Sele pichani kati akiwa amezungukwa na washabiki wake,huku akiwaimbia wimbo wake wa Karata Dume, shangwe na miluzi ilitawala uwanjani hapo wakati kampuni ya simu ya mikononi ya Airtel ilipokuwa ikizindua huduma yake mpya ya Airtel Money kwa wakazi wa mji wa Dodoma jioni ya jana.
No comments:
Post a Comment