HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, December 30, 2011

RAIS JAKAYA KIKWETE AONGOZA MAMIA YA WAKAZI WA JIJI LA DAR KUUAGA MWILI WA ALIYEKUWA MTANGAZAJI WA TBC MAREHEMU HALIMA MCHUKA LEO

Rais Jakaya Kikwete akipeana mkono na Mkurugenzi Mkuu wa TBC,Bw Clement Mshana wakati wa kutoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa mtangazaji wa TBC Taifa,Halim Mchuka leo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, kabla ya kwenda kuzikwa makaburi ya Msasani baada ya Sala ya Ijumaa.
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na kuwapa pole baadhi ya ndugu wa Marehemu Halima Mchuka,leo wakati alipofika kutoa heshima za mwisho.
Rais Jakaya Kikwete akiungana na viongozi wa msikiti wa Hospitali ya Taifa Muhimbili na wakazi wa jiji la Dar es salaam kuuombea dua mwili wa aliyekuwa mtangazaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) marehemu Halima Mchuka aliyefariki tarehe 29 Desemba mwaka huu jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Kikwete akitoa heshima za mwisho kuuaga mwili wa aliyekuwa mtangazaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) marehemu Halima Mchuka aliyefariki tarehe 29 Desemba mwaka huu jijini Dar es salaam. Mwili wa marehemu umezikwa leo katika makaburi ya Msasani jijini Dar es salaam.
Baadhi ya wafanyakazi wa Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo wakitoa heshima za mwisho kuuaga mwili wa aliyekuwa mtangazaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) marehemu Halima Mchuka wakiongozwa na Naibu waziri wa wizara hiyo Dkt. Fennela Mukangara (wa kwanza kulia) katika hospitali ya Taifa Muhimbili leo jijini Dar es salaam.
Baadhi ya ndugu na watoto wa marehemu wakiuombea dua mwili wa marehemu Halima Mchuka katika Hospitali ya Taifa Muhimbili leo jijini Dar es salaam.
Baadhi ya wanataaluma wa tasnia ya habari nchini na wafanyakazi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) wakiwa na majonzi mara baada ya kuuaga mwili wa marehemu Halima Mchuka aliyekuwa mtangazaji wa shirika hilo kwa takribani miaka 19 leo jijini Dar es salaam.
Mwili wa aliyekuwa mtangazaji wa TBC Halima Mchuka ukiingizwa ndani ya msikiti wa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya Ibada maalum kabla ya kupelekwa katika makaburi ya Msasani kwa ajili ya Mazishi.
Mwili wa aliyekuwa mtangazaji wa TBC Halima Mchuka ukiwekwa katika makao ya kudumu katika makaburi ya Msasani leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Emmanuel Nchimbi akishiriki mazishi ya aliyekuwa mtangazaji wa TBC marehemu Halima Mchuka leo jijini Dar es salaam katika makaburi ya Msasani.
Picha ya Marehemu ikiwa Juu ya Jeneza.
Mkurugenzi wa Zamani wa TBC,Bw. Tido Mhando akiwa kajumuika na waombolezaji wengine kwenye msiba wa Halima Mchuka.Picha na Aron Msigwa - MAELEZO na IKULU.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad