Mkurugenzi
wa Usafirishaji wa Mizigo wa Precision Air Bw. Elias Moshi akipanda mti
wa kwanza katika magereza ya Butimba jijini Mwanza. Kampuni hiyo
ikishirikiana na shirika la Mazingira na Uhifadhi Tanzania (TEMCO)
imeweza kupanda jumla ya miti 5000 katika eneo hilo.
Mkuu
wa Magereza ya Butimba Bw. Edson Yalimo akipokea cheti cha ushiriki
kutoka kwa Mkurugenzi wa Usafirishaji Mizigo wa Precision Air Bw. Moshi
na Mwenyekiti wa TEMCO Bw. John Masweta.
Wafanyakazi
wa shirika la ndege la Precision Air na TEMCO wakiwa katika picha ya
pamoja na utawala na maaskari wa magereza ya Butimba jijini Mwanza.
Precision
Air-shirika la ndege linaoongoza Tanzania ikishirikiana na Shirika la
Mazingira na Uhifadhi Tanzania (TECO) kwa pamoja wameweza kupanda miti
zaidi ya 5000 katika magereza ya Butimba leo jijini Mwanza kama namna ya
kuinua uhifadhi wa mazingira nchini.
Mkurugenzi
wa usafirishaji wa mizigo wa Precision Air Bw. Elias Moshi ambaye pia
alikuwa mgeni rasmi katika tukio hilo, alisema kwamba wakati Tanzania
ikisheherekea miaka 50 ya uhuru sasa, ni vyema tukawakumbuka na
kuwaandalia mazingira bora watanzania wa vizazi vijavyo ili na wao
waweze kufaidi matunda ya nchi yetu huko baadaye.
“Kupanda
miti si jukumu la serikali tu bali ni kwa watanzania wote kwa ujumla.
Ndo maana leo kama wafanyakazi wa Precision Air tumeamua kutoa
kipaumbele katika mazingira ili kuwa mfano kwa wananchi wengine,”
aliongeza.
Pia
Bw. Moshi alipendekeza serikali kupitisha mpango maalumu wa kupanda
miti na kukagua kama wamiliki mbali mbali wa ardhi wanafuata hiyo.
Akisisitiza kwamba ungekuwa mpango madhubuti ya kuhifadhi mazingira
nchini.
Wakati
huo huo, Mwenyekiti wa TECO Bw. John Masweta alisema kwamba katika
miaka 50 ya uhuru ya Tanzania ingependeza zaidi kama watu watasherehekea
kukiwa na uhakika wa mazingira bora pia.
“Kusema
tunashehereka miaka 50 ya uhuru tu peke yake haitoshi, bali ni vizuri
tukatafakari kuhusu namna tunavyoathiri mazingira yetu na tunaweza
kufanya nini ili kuweza kuyaboresha,” alisema.
Kwa
pamoja Bw. Masweta na Mkurugenzi wa Precision Air Bw. Moshi
waliishukuru utawala wa magereza ya Butimba kwa nafasi yakipekee
waliyopewa.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi wa Magereza ya Butimba Bw. Edson Yalimo alisema
ni jambo jema Precision Air walilofanya wakishirikiana na TECO
kuyakumbuka hata mazingira ya watanzania waishio magerezani.
“Tunawashukuru sana kwa kujali kwenu alisema,”alisema.
No comments:
Post a Comment