HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, December 29, 2011

Mvua yaharibu barabara za Mwanagati, Kitunda jijini Dar

Mambo vipi Mzee wa Mtaa Kwa Mtaa,

Natumai ni mzima wa afya na unaendelea vyema na libeneke.

Mie ni Mkazi wa eneo la Mwanagati, Kitunda, Dar es salaam ambapo barabara yetu huku imeharibika vibaya sana baada ya mvua kubwa iliyonyesha hivi majuzi na kuweza kutafuna njia zote na kubakia vipande,hali inayopelekea magari kupita moja moja huku upande mwingine ikisubiria lipite jingine na kufanya msongamano mkubwa. 

hivyo kupitia Libeneke la MTAA KWA MTAA tunaomba tufikishie ujumbe wetu wa kuhitaji msaada sie wananchi wa huku Mwanagati,Kitunda ili mambo yawe mswano kama ilivyokuwa awali.

ahsante sana na lidumu Libeneke la Mtaa Kwa Mtaa.

Mdau wa Mwanagati.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad